Njia 3 za kuweka App kwenye Android bila kutumia Google Play Store


Google Play Store inajulikana kama Soko la Android – jukwaa la usambazaji wa digitali kwa ajiri ya mifumo ya uendeshaji ya Android na digital media store inayoendeshwa na Google.

Google imewezesha kuwepo kwa uhifadhi mkubwa wa apps, games na vitu vingine, na karibu chochote unachokitaka, kinaweza kupatikana huko.

Hata hivyo, kuna nyakati ambapo unahitaji kuweka programu za Android kutoka nje ya Google Play Store. Google haifanyi kazi kama Apple linapokuja swala la kile kinachouzwa katika app store, lakini bado inaweza kupima viwango. Au labda unataka kuweka toleo la zamani la programu ambalo tayari unalimiliki kwa sababu linafanya kazi vizuri kwenye kifaa chako.

Hebu tuangalie baadhi ya njia unazoweza kuzitumia kuweka apps za Android bila kutumia Google Play Store

Ruhusu Uwekwaji wa Apps Kutoka Sehemu Zisizo Rasmi (Enable Unknown Sources)

Android app zilizo katika faili za APK pia zinaweza kupakuliwa kutoka nje ya Play Store (kama vile kupitia kivinjari chako cha wavuti). Hata hivyo, kabla ya kujaribu ku-install APK, lazima kwanza uidhinishe simu ili kuwezesha “Unknown Sources” (yaani, programu haipo kwenye Play Store).

Ili kufanya hivyo, nenda kwenye “Settings -> Security” na kubali sehemu iliyoandikwa¬† “Unknown Sources”, kisha bofya “OK” na “Trust”.

Tafuta Faili la App ya Android (APK) unalolitaka Kutoka Kwenye Intaneti

Unaweza kuwa tayari una tovuti inayoaminika ya kupakua APK. Ikiwa bado hujajua wapi unaweza kupakua apps zaidi,unaweza kutumia tovuti ya APKMirror , ambayo ni bora kwa APK zinazopatikana kisheria za matoleo ya programu za zamani za Play Store app, programu za bure, na zaidi.

Unaweza kushusha APK moja kwa moja kwa njia ya kivinjari cha simu yako, hapa utapokea ujumbe ukisema “This file may harm your phone.” . Usijali, ikiwa umepata faili kutoka APKMirror au faili nyingine kutoka kwenye tovuti unayoamini, simu yako itakuwa salama pia.

Pakua faili, kisha ufungue APK kisha Sakinisha (Install) programu yako mpya. Unaweza pia kupakua APK kupitia kivinjari kwenye kompyuta yako, ila utatakiwa kuhamisha faili kwenda kwenye simu yako kupitia microUSB au mtandao wa wireless na uiweka kutoka hapo.

 Mipangilio kwa kutumia Google Drive, Dropbox, na cloud services zingine

Pia, ukipakua APK kwenye kifaa kingine, unaweza kupakia (upload) kwenye cloud service kama Google Drive au Dropbox. Mara baada ya kukamilika, unaweza kuipata kupitia Google Drive or Dropbox. kwenye simu yako na kuifungua moja kwa moja kutoka kwenye huduma ya clouds, ili kuanzia kufanya installation.

Je ushawahi kutumia njia ipi kati ya hizi ? Na je makala hii imekusaidia ?

Toa maoni yako. Kumbuka kusambaza makala hii kwenye mitandao ya kijamii na kundelea kusoma mediahuru.com

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA