Linux ni mfumo wa uendeshaji kompyuta ambao hupatikana bure kabisa na katika ladha tofauti zinazofahamika kama ditros, kati ya distro maarufu sana duniani ni Ubuntu, Linux Mint, na fedora. Tofauti na Windows au Mac za Apple, kwenye Linux programu zote unazipata bure bila gharama yoyote.

Umaarufu wa Linux pia hutokana na uwezo wake wakutosumbuliwa na virusi (Computer Viruses) kama ilivyo kwenye Microsoft Windows, na uwezekano wa kupata msaada kwenye mtandao kwa urahisi na haraka sana.

Changamoto kubwa kwa wanaoanza ama kuhamia kutoka kwenye Windows na kuanza kutumia Linux, hasa Ubuntu, huwa ni kuzoea muonekano, na zaidi ni kupata programu (Softwares) ambazo alikuwa anazitumia kwenye Windows. Mfano, programu ya kuchapa (Microsoft Word) na nyinginezo nyingi.

SOMA NA HII:  Njia 6 za Jinsi Unavyoweza Kupunguza Matumizi ya Data kwenye Simu ya Android

Kwenye Linux kuna programu mbadala ya zile zilizoko kwenye Windows, hata hivyo zinaweza zisifikie kiwango na ubora wa zile za kwenye Windows, lakini kwa kiasi kikubwa zinaweza kukusaidia kufanya unayohitaji kama ambayo ungefanya kwenye windows

Kuna njia kadhaa zinazoweza kukuwezesha kutumia programu za Windows kwenye Linux, baadhi ya mbinu hizo ni:

1. Sanikisha programu kwa kutumia WINE au PlayOnLinux.

Hii programu inapatikana ndani ya ubuntu software center inaitwa WINE ikimaanisha “Wine is not Emulator” ambayo inakuwezesha kusanikisha (Install) programu za Windows kwenye ubuntu moja kwa moja kama vile iko kwenye Windows. Pia unaweza kusanikisha (Install) PlayOnLinux kwa ajili ya kuplay games za windows. Unaweza kusanikisha baadhi ya programu muhimu kama Microsoft Office, Adobe Photoshop, na nyinginezo nyingi.

SOMA NA HII:  Njia nyepesi za kubet na kufanikiwa katika Betting

2. Tumia virtualbox

Kwa kuwa Linux/Ubuntu inahakikisha usalama zaidi dhidi ya virusi vya kompyuta, na iko haraka kuliko Windows, unaweza pia ukaingiza Windows ndani ya Ubuntu kwa kutumia programu maalumu inayoitwa Virtual Box. Virtual Box inaweza kutengeza mfano wa kompyuta nyingine (Virtual Machine) ndani ya kompyuta yako uliyonayo, halafu ukaingiza windows na ukatumia programu zako unazotaka, pia unakuwa na uwezo wa kutumia OS zote mbili bila kuzima PC yako.

ZINGATIA: Hatua hii ya kutumia Virtual Box waweza pia kuifanya ndani ya Windows na ukasanikisha ubuntu ili kuijaribu na kujifunza kabla haujaamua kuitumia rasmi.

SOMA NA HII:  Listi ya Kampuni 10 za Kubeti Mpira Nchini Tanzania

3. Dual booting

Hii ni njia ya kusanikisha (Install)  OS mbili kwenye kompyuta moja na unakuwa unachagua ipi utumie unapowasha kompyuta yako. Hii haina shida yoyote kwa upande wa programu, ila ukitaka kutumia OS moja nyingine inakuwa imezima.

Bila shaka umeweza kupata angalau uelewa wa namya kutumia baadhi ya programu uzipendazo kwenye Windows ndani ya Linux. Kwa maoni, maswali na ama ushauri usisite kuniandikia kwenye fomu ya maoni hapo chini.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako