[Mwongozo] Jinsi ya kutumia Akaunti mbili za WhatsApp kwenye Kompyuta yako


Tutakuonyesha njia rahisi sana ya kutumia akaunti mbili au zaidi kwa wakati mmoja kwenye WhatsApp Web kwenye kompyuta yako.

Je! Umewahi kujiuliza itakuwa pale utakapoweza kutumia akaunti nyingi za WhatsApp kwa wakati mmoja kwenye kompyuta yako? Inaweza kuonekana kama haiwezekani kwa kitu kama hicho kutokea lakini toleo la WhatsApp kwajili ya PC limefanya iwe rahisi zaidi kuamini jambo hili. Sasa mtu yeyote anaweza kutumia akaunti zaidi ya moja ya Whatsapp kwenye toleo la kompyuta wakati huo huo.

akaunti

WhatsApp – Programu Bora ya Kutuma Ujumbe

Bila shaka, WhatsApp imekuwa mojawapo ya programu maarufu zaidi za ujumbe wa papo kwa papo (instant-messaging apps), na ina watumiaji zaidi ya bilioni 1.5. Mfalme asiye na mpinzani wa mitandao ya kijamii huduma yake ya ujumbe wa papo hapo inafikisha meseji zaidi ya milioni sitini zinazotumwa kila siku.

Mwaka 2014, Facebook iliponunua kampuni ya Whatsapp, ilianzisha toleo la mtandao la huduma hiyo ya ujumbe wa papo hapo, kwa lengo la kuzalisha faida zaidi na kupanua msingi wake wa watumiaji. Ikiwa bado hujui, toleo la wavuti la Whatsapp linaruhusu watumiaji kufikia akaunti zao za WhatsApp kwa kutumia PC zao.

Kuna maoni mengi kutoka kwa watu ambao wana akaunti zaidi ya moja ya WhatsApp. Wakati tunajua tunaweza kutumia akaunti nyingi kwa wakati mmoja kwenye simu janja lakini wengi wetu hatujui unaweza kufanya hivyo kwenye PC pia. Ndio, kuna njia rahisi ambayo itakuwezesha unaweza kutumia akaunti nyingi za WhatsApp kwenye kompyuta yako bila shida yoyote.

Ikiwa hujui jinsi ya kutumia WhatsApp web, basi hebu tufafanue kwa haraka. Ili kufikia WhatsApp web,, unatakiwa kuwa na akaunti ya WhatsApp inayofanya kazi kwenye simujanja yako pamoja na uunganisho wa intaneti kwenye vifaa vyote. Zaidi ya hayo, unapaswa kuwa na toleo la sas la kivinjari cha chaguo lako mwenyewe. Kwa mfano, ikiwa unatumia Google Chrome kama kivinjari chako , basi unatakiwa kuwa na toleo lake la hivi karibuni.

Kutumia Akaunti nyingi za WhatsApp kwenye Kompyuta

Hapa ni jinsi gani unaweza kutumia akaunti nyingi za Whatsapp kwenye kompyuta yako.

Hatua ya 1:

Jambo la kwanza, fungua kivinjari cha wavuti (web browser) kwenye kompyuta yako na nenda kwenye http://web.whatsapp.com. Baada ya hapo, fungua programu kwenye simu janja yako au tablet.

Hatua ya 2:

Mara baada ya kufungua tovuti kwenye kompyuta, QR code itaonekana kwenye skrini ya kompyuta na simu janja yako au tablet ili uweze kuanza kutumia akaunti ya WhatsApp. Kwa wale ambao hawajui jinsi ya kuunganisha mtandao wa Whatsapp na kompyuta yako, bonyeza alama ya nukta tatu zilizopo juu upande wa kulia wa programu na kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa WhatsApp web. Hapo ndipo ambapo utaweza kuscan QR code kwenye skrini ya kompyuta. Mara baada ya code kusoma vizuri, unaweza kuanza kutumia akaunti yako kwenye toleo la kompyuta.

Hatua ya 3:

Hatua inayofuata inatakiwa ufungue ukurasa mpya katika kivinjari sawa ili utumie akaunti nyingine ya WhatsApp kwenye toleo la kompyuta.

Hatua ya 4:

Unatakiwa ku-paste kiungo (link) hiki kwenye ukurasa uliofunguliwa http://dyn.web.whatsapp.com na kisha bofya Enter. Ukifunguka ukurasa unaotaka, utapata tena QR code kwenye skrini.

Hatua ya 5:

Rudia hatua za mwanzo kwa ku-scan QR code na akaunti yako nyingine ya WhatsApp na Hongera! Umefanikiwa.

Hii inakuwezesha kufikia akaunti mbili za WhatsApp kwenye kivinjari sawa. Je, sio rahisi kufuata mwongozo huu? Kwa kufuata mchakato huo tena, unaweza pia kutumia akaunti ya tatu ya Whatsapp katika kivinjari chako cha wavuti.

Tunatarajia mwongozo huu umekuwa na msaada mkubwa kwako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA