Sambaza:

Watazamaji wataanza kuona mechi zote za Klabu bingwa barani Ulaya mubashara kupitia mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 2 duniani.

Mwanzilishi na CEO wa mtandao wa Facebook, Mark Zuckerberg

Kampuni ya Facebook imefikia makubaliano na Kampuni ya 21st Century Fox Inc kutumia Channel ya Fox Sports kuonesha mechi za Klabu bingwa barani Ulaya kupitia mtandao wake wa Facebook kuanzia msimu mpya ujao unaotarajiwa kuanza mwezi Septemba.

Kwenye makubaliano hayo Facebook itachukua fedha zote za matangazo yatakayoingia kipindi mechi hizo zikirushwa ingawaje kampuni ya Fox haijaweka wazi ni kiasi gani imelipwa na Facebook.

SOMA NA HII:  Facebook imesai deal kubwa na Universal Music

Mtandao wa Facebook umefikia maamuzi hayo baada ya kuona idadi kubwa ya watumiaji wake hufuatilia michezo.

“Mpira wa miguu unakuwa na msisimko zaidi unapokuwa live lakini vipi kama ukiwa peke yako huku ukihitaji maoni ya wenzio au kupongezana na mashabiki wenzio? hii tumeona ni vyema tuwaletee wateja wetu kitu ambacho wataangalia live na kutoa maoni yao hapo hapo hii itapunguza gharama kwa watumiaji pia itakuwa ukomo wa TV“,amesema Sheryl Kara Sandberg Afisa Mkuu mwendeshaji wa Kampuni ya Facebook Inc.

Kwa upande wa Kampuni ya FOX wao wamesema tayari walianza mapema kuwapa vionjo wateja wao hususani wafuatiliaji wa kurasa zao za Fox Sport kwa kuwapatia kipindi cha  weekly soccer show na kuahidi kuwa kwa sasa vitu vyote vitakuwa live na watafunga baadhi ya channel zao zilizokuwa zinaonesha michuano hiyo.

“Kuna mechi nyingi sana zinachezwa Uingereza na ligi ya Hispania kuliko hata idadi ya Channel zetu ambazo tunazitumia kurusha mechi hizo lakini kwa sasa mtumiaji wetu atapakua App moja tu na kutazama mechi azipendazo”,amesema David Nathanson, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Biashara cha Fox Sports.

Mradi wa Facebook na vituo vikubwa vya Runinga vinavyoonesha michezo kuweka Video zao kwenye mtandao huo umekuwa na mafanikio makubwa tangu uanzishwe miaka mitatu iliyopita na umepelekea Kampuni hiyo kuongeza Feature ya ‘Video Live’.

Kwa hili la kuonesha mechi kupitia Facebook tunaimani Fox watawafikia mamilioni ya watazamaji wake kwani watu wengi kwa sasa wanatumia muda mwingi mitandao kuliko kwenye Runinga“,amesema Dan Reed mkuu wa kitengo cha michezo wa Kampuni ya Facebook.

Kwa kuanza Facebook wataanza kuonesha mechi za Klabu bingwa barani Ulaya kwa nchi za Amerika ya Kaskazini na baadae kusambaa duniani kote.

SOMA NA HII:  Kampuni ya mawasiliano ya Zantel kuigeuza Tanzania kuwa kitovu cha Tehama

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako