Simu

Kufufuka Kwa Legend: Kutana Na Nokia 3310 (2017)

Katika makala za nyuma tulitoa taarifa kwamba Nokia watatangaza ujio wa Nokia 3310 (2017) katika MWC, na maneno hayo ni kweli, wamefanya hivyo. Simu mpya ya kisasa ya 3310 inaendeshwa na programu ya Nokia Series 30+, 2.4 inch QVGA polarized ikiwa na kioo chenye rangi, kamera ya 2-megapixel, na pia ina micro SD slot. Uwezo wa kuhifadhi wa ndani ni 16MB huku ukiwa na uwezo wa kuweka microSD hadi 32GB. Inaunganishwa na mtandao kupitia 2G na inakuja na “200 mAh battery”.

Oh, pia inakuja na jack 3.5 mm!

3310 (2017) ina mvuto zaidi wa rangi, ndani na nje, ukilinganisha na toleo la zamani la Nokia 3310 la mwaka 2000. Rangi nne tofauti ni nyekundu, njano, bluu na kijivu. Vitufe ni vyeupe. Huwezi kuichanganya na simu nyingine yoyote, ina tambulika kama Nokia, na HMD (kampuni inayotengeneza simu zenye chapa ya Nokia) imeweka pia mchezo wa Nyoka wa kisasa kwenye simu hii.

Simu hii ina uwezo wa kuingia mtandao, kwa njia ya Opera Mini. Kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, 3310 mpya inakuja na betri linalokaa muda mrefu. HMD ina mpango wa kufanya Nokia 3310 mpya ipatikane sokoni mwanzoni mwa mwezi wa sita mwaka huu. Bado hatuna uhakika kama simu hii itafika kwenye masoko ya  Afrika.

SOMA NA HII:  Simu Mpya za Google Pixel 2 Zimevuja Kabla ya Kutoka (Bei+ Picha)

Picha kwa hisani ya Verge

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.