Idadi ya Kushusha App Duniani Imefikia bilioni 175 mwaka 2017, Fahamu Nchi Inayoongoza


Idadi ya kushusha app duniani imeongezeka hadi kufikia bilioni 175, kutokana na kuuongezeka kwa watu wanaoshusha apps katika nchi kama China, India, Brazil na Urusi, Kwa mujibu wa ripoti mpya ya App Annie iliyotoka hivi karibuni. India sasa inashika nafasi ya pili kwa kuwa na downloads nyingi, imeizidi Marekani, ambayo ipo nafasi ya tatu. China inaendelea kushikiria nafasi ya kwanza.

Utofauti wa idadi ya kushusha App kwenye ripoti ya App Annie ambayo ni bilioni 175 na bilioni 91.5 kwenye ripoti ya hivi karibuni ya Sensor Tower inaweza kuonyesha kwamba data hizi zilikisiwa. Sensor Tower ilitumia iOS App Store na Google Play. Hata hivyo, App Annie, ilihusisha pia huduma zingine za kupakua App  za Android kwenye uchunguzi wake – Ndio maana imehusisha na China, nchi ambayo Google Play haifanyi kazi.

India imeshika nafasi ya pili kwa wingi wa downloads hii imebadilisha mtazamo wa soko la app duniani.

Downloads nchini humu zimeongezeka kwa asilimia 215 ndani ya miaka miwili iliyopita, ikifananishwa na asilimia 125 ya ongezeko nchini China, na kushuka kwa asilimia 5 nchini Marekani.

App Annie imegundua kuwa ongezeko la matumizi ya apps chini India yamechangiwa na kuanzishwa kwa huduma huduma ya 4G iliyozinduliwa na Jio mwezi septemba 2016, ambayo inawewezesha watumiaji kuingia mtandaoni kwa idadi kubwa.

Ingiwa Marekani bado ni soko kubwa la apps, App Annie inasema bado kuna ukuaji mkubwa wa soko la apps katika maeneo mengine

Kwa mfano, uchunguzi huo umebaini kwamba, Kwa Marekani watumiaji wanashusha apps 3 kwa mwezi, na angalau asilimia 70 wanapakua app moja.

Ripoti pia inaonyesha app zilizofanya vizuri kwa mwaka 2017 zikiwa katika makundi tofauti kam fedha, biashara, video streaming, masuala ya utalii, gaming, na mitandao ya kijamii. Unaweza kuomba ripoti kamili kwenye tovuti ya App Annie.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA