Sambaza:

Moja ya changamoto ambayo watumiaji wa android wanapaswa kuishughulikia ni kupunguza matumizi ya data kwenye simu zao za mkononi kuwa katika  kiwango cha ‘matumizi ya kawaida.’

Katika kesi hii, matumizi ya kawaida yanahusu kuvinjari mtandao, kupakua na / au kupakia vitu mtandaoni.

Mbali ya matumizi ya kawaida, kifaa chako cha Android kitapakua mara kwa mara matangazo (video na picha), kusasisha programu (update apps) na kutuma takwimu za matumizi kwenye seva.

data kwenye simu

Njia 6 za Kupunguza matumizi ya data ya simu kwenye Android

Kwa hiyo unawezaje kuhakikisha kwamba kifaa chako hakipotezi data nyingi kwa haraka nje ya matumizi ya kawaida ? Hivi ndivyo unavyoweza kupunguza matumizi ya data:

Sitisha “Background Apps”.

Simu janja zote zinauwezo wa kuendesha apps zadi ya moja yaani unaweza kucheza game huku unapokea msg za whatsapp, app ambayo inaendelea kufanyakazi ingawa wewe umefungua app nyingine inatajwa kuwa ni background app.

Programu nyingi zitatuma na kupokea data kutoka kwenye seva hata wakati ambao huzitumii mbele ya skrini ya simu yako.

SOMA NA HII:  Tech!! Apps 8 Unazoweza Kuzitumia Kugeuza Windows Pc Kuwa Wi-fi Hotspot

Kiasi cha data kilichotumwa au kupokelewa kitatofautiana kutoka programu/app moja hadi nyingine; baadhi zitakuwa na kiwango cha KBs chache tu wakati nyingine zinaweza kutumia MBs za kutosha.

Ili kuzuia matumizi ya data kwenye background app , fungua mipangilio (settings) , chagua matumizi ya data (data usage), gonga kwenye mipangilio ya menyu (menu settings) na uchague ‘restrict background data.’

Zima “Auto-Update” ya Apps kwenye Data ya Simu ya Mkononi (Mobile Data)

Uboreshaji apps kutoka Hifadhi ya Google Play hutumia kiwango kikubwa cha data kwenye simu. Jinsi ulivyoweka apps nyingi; ndivyo data zaidi itatumika kuzisasisha.

Kwa bahati nzuri na kwa hekima ya Google wamegundua hii inaweza kuwa shida kwa baadhi yetu na kuamua kuweka chaguo la kuzima auto-updates (disable auto-updates)

Ili kuzima auto-update, fungua app ya Google Play Store, kufungua menyu ya mipangilio (settings menu), chagua chaguo la Auto-update apps na kisha chagua ‘Do not auto-update apps.’

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Infinix Note 4 Pro na sifa zake

Hii inamaanisha utatakiwa kuangalia ikiwa kuna sasisho kwenye apps na kuzipakua mwenyewe.

Sasisha (update) Apps kupitia Wifi

Kusasisha apps zilizomo kwenye simu yako ni muhimu sana, kwa sababu usipofanya hivyo itakufanya usipate  maboresho mapya ya uzoefu bora wa mtumiaji na sasisho muhimu za usalama.

Badala ya kuzima auto-update, chagua chaguo la ‘Auto-update apps over Wi-Fi only’. Hii inahakikisha kwamba kifaa chako lazima kitafanya sasisho la apps kiotomatiki wakati wowote unapounganishwa na Wi-Fi hotspot ya bure.

Zima Data wakati wa kucheza Game

Game nyingi za bure zitakuletea matangazo wakati wa gameplay au wakati wowote unaposimamisha game yako. Baadhi ya matangazo hayo huja katika mfumo wa video.

Ili kuepuka hili, zima data ya simu yako kabla ya kufungua app ya game.

Pakua Apps za kulipia

Apps nyingi zina matoleo ya kulipia ambayo hayana matangazo. Ili kupunguza matumizi ya data kutokana na matangazo, hamia kwenye toleo la kulipia kupitia orodha ya mipangilio ya app husika.

SOMA NA HII:  Bei ya Infinix Note 3 X601 Sifa na Uwezo wake Tanzania

Mara tu unapolipia app utafurahia matumizi ya apps bila kuingiliwa kwa sababu hutaona tena matangazo.

Tumia kivinjari kinachopunguza matumizi ya data

Kivinjari cha simu (mobile browser) ambacho kinafungua kurasa katika fomu yake kamili kitatumia data zaidi kuliko kile kinacho compresses kurasa hizo.

Wakati apps kama Google Chrome zinataka uweke kwa hiari chaguo hili, zingine kama Opera na Opera Mini huja na mfumo huu moja kwa moja kama default.

Opera Mini pia inakuwezesha kuweka compression ya data kwa kiwango cha extreme, high, au automatic.

Ili kuwezesha data saver kwenye Chrome, fungua orodha ya mipangilio na shuka chini hadi kwenye Data Saver. Chagua chaguo hilo.

Ili kuzima data saving kwenye Opera Mini, bonyeza icon ya Opera ili kufungua orodha kuu na uchague ‘Data Savings’ . Chagua Off ili kuzuia compression ya data.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako