[Video] Sasa utaweza kupima chakula kwa simu yako kabla ya kula


Kila siku Tunasema asante kwa teknolojia kwa sababu ya vitu vizuri ambavyo tunakutana navyo vikikufikia na kurahisisha mambo mengi kwa sababu tu wataalam wamekaa na wamebuni kitu kizuri !!

Unaambiwa ni suala la kukaa tayari wakati wowote kuanzia sasa tutakuwa na simu zenye uwezo wa kufanya scanning chakula na kutoa majibu kwamba kwenye chakula kuna nini na nini…

Kwa sasa kuna kifaa kinaitwa SCiO scanner ambacho ni kidogo tu hivi na kina uwezo wa kufanya scanning kugundua vitu vingi kama kiasi cha sukari kwenye chakula, au mafuta, chumvi, kemikali na vitu vingine… hiki kifaa kimeingizwa kwenye list ya ugunduzi mkubwa uliofanywa kwa mwaka 2015.

Ukiwa na SCiO scanner kama ni mtu mwenye tatizo la kisukari au presha inaweza kumsaidia pia kwa ajili ya kuweza kudhibiti kula vyakula ambavyo havitakiwi kwa wakati akiwa kwenye hali ya kuumwa.

Video ya kifaa chenyewe hii hapa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA