Sambaza:

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Research ICT Africa iliyoandaliwa kwajili ya Mozilla (Via MyBroadBand), gharama za kununua data ni kizuizi kikuu kwa matumizi ya intaneti nchini Afrika Kusini.

Utafiti huo uliwauliza maswali watu mbalimbali kwa vikundi kwa kuzingatia kutoka maeneo ya jiji, miji ya kawaida, vijijini, na vijiji vya ndani kabisa nchini Afrika Kusini pamoja na nchi nyingine za Kiafrika na kugundua kuwa gharama ya kupata data na kasi yake iliwaacha watu wengi waliohojiwa wafadhaike. Utafiti huo pia umebaini kuwa kama matokeo ya bei ya vipande (bundles) vya kila mwezi vya data, washiriki wengi walichagua vifurushi vidogo vinavyotumika haraka, na bundles zinazokaa kwa kipindi vifupi kuliko cha mwezi, pia walitumia “subsidized data services” kama moja ya njia za kuokoa fedha- Njia hizo ni pamoja na:

  • Matumizi ya kadi nyingi za SIM ili kufurahia promotions, ubora wa mapokezi, au bei bora za huduma iliyotolewa.
  • Kwa mfano, mabasi mengi nchini Rwanda sasa hutoa huduma ya wifi, na washiriki waliripoti kuwa tayari kusubiri basi ambayo ilikuwa imewezeshwa na Wi-Fi.
  • Kujiunga na hotspots za simu. Nchini Afrika Kusini na India, watumiaji sio tu wanashirikishana data lakini pia promotions na ofa zingine zinazotolewa kutoka mtandao moja hadi mwingine.
  • Maombi ya malipo yaliyopatikana (ambapo watumiaji wanapakua, wanatumia, au kushirikisha app inayotangazwa kwa kurudishiwa data za simu / salio). Utafiti unaonyesha kwamba watumiaji wengi wanapenda kucheza mfumo wa kupata salio kadri iwezekanavyo na kuacha application unayolipwa unapoitumia.
SOMA NA HII:  Google Sasa Kuzuia Matangazo Kupitia Kisakuzi Kipya cha Chrome

Kwa hiyo, hili ni jambo la Afrika? Labda, lakini mimi binafsi nadhani Tanzania hatuendani na nchi zingine kabisa.

Kulingana na ripoti hii, Tanzania ina kiwango cha bei nafuu kwa data 1 gig ni takriban dola za marekani 0.89 ikilinganishwa na Afrika Kusini ambayo ni bei ya dola 5.26 za Marekani. Masoko mengine makubwa kama Misri, Kenya, na Nigeria wana bei kubwa zaidi za data kuliko Tanzania.

Kwa Habari Zaidi Na Maujanja Mbalimbali Ya Teknolojia Endelea Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwani Daima Tunaaminika Katika Teknolojia!


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako