Jinsi ya Kununua Simu Sahihi kwa Matumizi Yako


Simu za mkononi zimekuwa kitu muhimu kwenye maisha yetu. Zinatusaidia kuendelea kuwa karibu na jamii inayotuzunguka, kuchukua picha, kusikiliza na kuangalia video za muziki tunazozipenda, kuhariri nyaraka mbalimbali na zaidi.

Kwa kuwa simu ni kama “marafiki zetu wa karibu”, kuna mambo kadhaa unatakiwa kuzingatia wakati wa kununua simu inayokidhi mahitaji yako. Swali kubwa ni – Unanunuaje simujanja sahihi?

Watu wengi wanaangalia bei ya simu kama sababu kuu wakati wanatafuta kifaa kipya. Wakati wa kununua simujanja mpya, kuna mengi zaidi ya kuzingatia kuliko bei tu. Unaweza kuwa na pesa nyingi, lakini hiyo haina maana unapaswa kununua kifaa cha gharama kubwa zaidi kwenye soko.

Yafuatayo ni mambo muhimu kuzingatia wakati wa kununua simujanja mpya.

Fahamu unachotafuta

Kabla ya kununua simujanja mpya unapaswa kujiuliza swali hili, Ninatafuta nini?

Je! Unatafuta simu iliyoingia kwenye soko hivi karibuni ?, Je, unataka simu kubwa ?, Unataka kamera nzuri? . Kujua unachotaka ni muhimu sana wakati wa kuamua ni simu gani unayotaka kununua. Hakuna haja ya kuwa na simujanja yenye kamera bora huna mpango wa kupiga picha yoyote.

Mfumo wa Uendeshaji

Mfumo wa Uendeshaji wa simu yako ni mfumo ambao simujanja yako inatumia kufanya kazi. Wakati wa kuchagua mfumo wa uendeshaji, unapaswa kuzingatia jinsi OS husika inavyofanya kazi – Je! Unaweza kuhariri na kutuma nyaraka? Je! Unaweza kuchukua screenshots? Je! Unaweza kuiboresha zaidi? Unapaswa pia kufikiria upatikanaji wa programu zake. Kuna Mifumo ya Uendeshaji ambayo inapokea programu miaka baada ya nyingine. Android ni Mfumo wa Uendeshaji maarufu zaidi na unapendekezwa sana kwa vile unatoa ubunifu zaidi na una vipengele vingi kuliko washindani wake.

Bidhaa/Brand

Unapotaka kununua simu mpya, unapaswa kuzingatia brand / kampuni inayozalisha kifaa. Kwa nini ninasema hili? Bidhaa maarufu zinasifika kwa kutoa msaada katika suala la warranty,, vifaa, sasisho za programu na ukarabati wa bidhaa. Hutakiwi kwenda China ili uweze kubadilisha skrini iliyoharibika.

Utendaji

Kwa lugha nyepesi unaweza kusema urahisi wa kutumia na kasi ya simu yako. Linapokuja swala la utendaji, daima angalia kifaa chenye RAM nzuri, hifadhi nzuri na processor nzuri. RAM ni sehemu ambayo inaweka vitu sawa kwa ajili ya processor kuwasilisha kwako. Angalia kwa njia hii. Ikiwa una RAM kubwa, unaweza kuweka vitabu vingi ndani yake kwa wakati mmoja. RAM zaidi ina maana unaweza kuendesha programu nyingi zaidi kwa wakati mmoja (multi-tasking). Usinunue simu yoyote ambayo ina chini ya Gb 2.

Processor ni injini ya kifaa chako. Injini bora ni utendaji bora. Daima angalia ubora wake. 2.0 Ghz dual core ni bora zaidi ya 1Ghz  dual core.

Hifadhi ya ndani (Internal storage) ni muhimu sana kwa sababu programu nyingi zinawekwa kwenye hifadhi ya ndani ya simu. Simujanja nyigi zinakuja na hifadhi ya ndani ya wastani wa 4Gb chini ya hapo simu hiyo haifai.

Ukubwa wa Skrini

Simu zenye Skrini zenye Ukubwa Tofauti

Angalia ukubwa wa skrini kama shamba. Skrini kubwa, ndivyo unavyoweza kufanya vitu vingi zaidi juu yake. Ikiwa unatumia simu yako kwajili ya kutuma na kupokea pesa kupitia M-pesa basi huhitaji simu yenye skrini ya 5.5 inchi. Ikiwa wewe ni mpenzi wa Instagram au unataka kuhariri nyaraka kwenye simujanja yako basi ningependekeza skrini kubwa. Skrini ya 4-4.3 ni ndogo, skrini 4.5 hadi 4.8 ni wastani wakati yoyote juu ya inchi 5 inachukuliwa kuwa kubwa.

Betri na Kudumu

Betri kubwa ni bora. Angalia idadi. Betri zinapimwa kwa Milliamp Hours (mAh). Betri ni muhimu sana kwa vile simu yako haina maana kama muda wote imezima. Pia hutaki kubeba power-bank kila mahali unapoenda. 1500mAh ni kiwango cha wastani ambapo 2000mAh na kuendelea ni bora zaidi.

Durability ni muda gani simu yako inaweza kudumu. Rafiki yangu moja alinunua simu mpya na siku ya pili, skrini tayari ilianza kuwa na mikwaluzo. Watu wachache sana wanaweza kubadilisha simu kila mwezi kwa hiyo unatakiwa kutafuta simu inayodumu.

Jaribu angalau kununua simu yenye ulinzi wa skrini . Hii itaokoa gharama ya kununua screen protectors kila mwezi. Ninasisitiza juu ya ulinzi wa skrini. Kabla ya kununua simu mpya, jaribu kutumia google na uangalie kama ina ulinzi wa skrini.

Kamera

Ubora wa kamera ni suala ambalo linajadiliwa sana lakini unachotakiwa kujua ni kwamba megapixels ni bora zaidi kwenye karatasi. Nyingi kama sio simujanja zote huja na megapixels 4 au zaidi. Kuwa na kamera ya megapixel 6 ni vizuri na kamera ya megapixel 9 ni bora zaidi. Ubora wa kamera ni muhimu sana kwa sababu hata kama hupendi kuchukua picha kila siku, muda utafika unapaswa kuchukua picha na utachukia kuwa mtu anayeboa kila wakati.

Sababu nyingine

Teknolojia ya mtandao pia inapaswa kuzingatiwa. Simu zote za kawaida zimewezeshwa 3G. Watoa huduma mbalimbali sasa wanatoa huduma ya 4G hivyo kama wewe ni aina ya mtu ambaye anahitaji uunganisho wa haraka wa mtandao basi unapaswa kununua simu ya 4G. Ikiwa unaishi katika eneo ambalo hakuna uunganisho wa mtandao wa 4G basi haipaswi kuwa na haraka kununua simu ya 4G.

Vipengele vya ziada kama wireless charging, curved screens pia vinaweza kuzingatiwa ikiwa ni vya muhimu kwako.

Bei

Bei ya kifaa inapaswa kuwa sababu ya mwisho. Kwa nini ninasema hili? ikiwa kwenye akili yako umeweka kwamba unatakiwa kununua simu ya bei chini ya kiasi fulani unaweza kununua simujanjae ambayo huihitaji.

Fahamu aina ya vipengele unavyohitaji kwanza ili hata ikiwa una kiasi kidogo cha fedha unaweza kulinganisha sim zilizopo kwa aina hiyo ya bei hivyo utaweza kuchagua bora kati yao.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA