Jinsi ya kununua simu na kutambua ubora wake


Unapotaka kununua simu (smartphone) mpya kupitia mtandao ama maduka ya kawaida kuna vitu ambavyo ni muhimu kuzingatia ili kujua uwezo wa simu na ubora wake. Mbali na kuangalia uwezo wa kamera ya simu husika, betri na vitu vingine, Mediahuru tumekusogezea mambo muhimu ya kuzingatia unapotaka kununua simujanja. Soma hapa ili kujua mambo hayo muhimu.

kununua simu

Njia rahisi za kununua simu na kutambua ubora wake

Simu za Kuepuka

Epuka kununua simu ambazo zina zaidi ya miaka 2, kuna simu nyingi madukani lakizi zingine tayari zimepitwa na wakati na hazina teknolojia ya kisasa zaidi. Hivyo ni vyema kununua simu iliyotengenezwa hivi karibu kwa sababu inakuja na teknolojia inayoendana na mazingira ya sasa. Kuna simu mpya nzuri zinatoka kila siku na zinapatikana kwa bei nafuu.

Vipengele Unavyotaka

Angalia ili kuhakikisha simu ina sifa muhimu zinazofaa kwako. Jaribu kupata moja yenye angalau 64GB ya hifadhi ya ndani (kiwango cha chini ya 32GB), pamoja na sehemu ya kuweka memori kadi (MicroSD slot)  ili uweze kuongeza hifadhi zaidi baadaye. Uwezo wa kuzuia maji wa IP67 unapaswa kuwa kiwango cha kawaida kwenye vifaa vingi na utaona manufaa yake siku utayodondosha simu yako bafuni. Simu nyingi hazina sehemu ya headphone (3.5mm headphone jacks) , hivyo hakikisha yako ina sehemu hiyo. Pia simu unayotaka kununua  inatakiwa angalau kuwa na Snapdragon 630 processor na 4GB ya RAM. Inapaswa pia kutumia Android 8.0 Oreo (2017) na kuendelea.

Kuwa Mjanja, Fanya Mahesabu

Simu zinapozinduliwa huwa zinauzwa kwa bei kubwa sana, hivyo unaweza kusubiri kwa miezi kadhaa ili ishuke bei ama unaweza kununua simu bora zinazouzwa kwa bei ya punguzo (ofa) na kampuni za simu za mkononi . Pia unapoenda dukani linganisha bei kwenye maduka matatu hadi matano ili kuepuka kuingizwa mjini na wajanja.

Nunua Simu Ambayo Haijafungwa

Unaponunua simu ambayo haijafungwa, unaweza kubadili laini kwa urahisi mtandao mwingine unapotoa ofa bora zaidi inayoendana na matumizi yako. Je, pale unaponunua simu iliyofungwa na mtandao fulani wa simu, inakuaje siku umeamua kubadilisha mtandao wa kutumia?

Hayo ndio baadhi ya mambo ambayo unapaswa kuzingatia unapotaka kununua simu yako kwa mara ya kwanza, ni muhimu kuzingatia haya kwani itakupa uwezo wa kuchagua simu yenye sifa nzuri.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA