Wakina dada sasa mnaweza kununua Mikoba ya Kisasa Ebay mtandaoni kwa usalama zaidi


eBay imezindua huduma mpya ya Uthibitisho (Authenticate service), ambayo inathibitisha, inabainisha, na kuuza mikoba ya kisasa zaidi kwa niaba ya wauzaji.

Huduma ya uthibitishaji imeundwa kusaidia wanunuzi kununua mikoba ya bei ghari kwenye soko hilo la mtandaoni kwa kujiamini.

“Wauzaji wa eBay sasa wanaweza  kutumia huduma hii kuorodhesha mikoba ya kifahari na wallets za thamani kuanzia $ 500 + na kupata 80% ya bei ya mwisho ya kuuza wakati wa kuuza mikoba- eBay.

Makampuni yanayojihusisha na biashara hiyo ni pamoja na Balenciaga, Burberry, Céline, Chanel, Christian Dior, Fendi, Goyard, Gucci, Hermès, Louis Vuitton, Prada, na Valentino.

Kwa muda maalumu, huduma itakubali mikoba yenye thamani ya $ 250 + na wauzaji watapata 90% ya bei ya kuuza.

“Kwa wanunuzi wa eBay, wanaweza kununua zaidi mikoba ya kifahari kwa ujasiri kwa kutambua kwamba vitu vyenye alama ya Uthibitisho vinakuwa na dhamana ya fedha (money-back guarantee) ya asilimia 200.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA