Opera CEO: Kuiuza Opera kwa Kampuni za China Haikuwa Uamuzi Wetu


Baada ya miezi kadhaa ya uvumi, Opera hatimaye ilithibitisha wiki mbili zilizopita kuwa bodi yake imekubali ofa ya kuuza bidhaa yake kwa muungano wa makampuni ya Kichina kwa bei ya dola bilioni 1.2.


Lars Boilesen, Mkurugenzi Mtendaji wa Opera, na Håkon Wium Lie, CTO wa kampuni hiyo na mwanzilishi wa cascading style sheets (CSS) hawakuweka wazi uuzaji ulivyopendekezwa na kwa mujibu wa mahojiano waliofanya kwenye mkutano wa MWC  2018 uuzaji bado haujakamilika. Wote wawili walibainisha kuwa uuzaji ulikuwa matokeo ya matakwa ya bodi na wahisa na si maamuzi yao wenyewe.

Mkurugenzi Mtendaji wa Opera

Katika mahojiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Opera alisema:

“I have been working for Opera since ’99, Håkon ’98,” Boilesen said. “He’s No. 8; I’m No. 16. We’ve been with Opera for many years. We got listed on the Stockholm stock exchange in 2004. So basically, the shareholders — they decided to initiate this process. It was kind of their decision. It wasn’t our decision.”- Lars Boilesen.

Opera sasa imeuza baadhi ya hisa zake  kwa kampuni za kichina kama kampuni ya gemu za simu ya Kunlun, kampuni Qihoo ya 360, na Yonglian Investment.

Kivinjari Kipya Kwajili ya Marekani

Ili kukua zaidi, Opera inaamini inahitaji mshirika mwenye nguvu katika masoko haya ambapo bado ina mengi ya kuboresha ili kufanikiwa zaidi – lakini hiyo haina maana kampuni inaachana na soko la Marekani. Boilesen na Wium Lie wamesema kwamba wangependa kupata sehemu zaidi ya soko nchini Marekani na walithibitisha kuwa Opera inatengeneza kivinjari kipya mahsusi kwa lengo hili.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA