Namna ya kuhamisha Apps Zisizohamishika kwenda kwenye Memori kadi


Simujanja au tablet nyingi zilizopo madukani hasa zinazotumia android OS zina sehemu ya kuweka Memori Kadi (memory card slot) kumwezesha mtumiaji kuongeza nafasi ya ziada ya kuhifadhi data. Ikiwa simu yako ina Diski ujazo (Internal Storage) ndogo, kuweka games au apps kwenye simu hiyo inaweza kupunguza utendaji wake.

Memori kadi

Ili kuepuka hali hii, unatakiwa kuhamishia Apps na Games katika Memori kadi ambayo umeiweka kwenye kifaa chako.

Kwa sio simu zote za Android zinakuwezesha kuhamishia apps ama games kwenye memori kadi kwa kutumia njia ya kawaida, watumiaji wengi wameomba niwasaidie njia nyingine ya kuhamisha apps. Hapa nimekusogezea maelezo ya kina kuhusu app ya Lucky Patcher ambayo ina uwezo wa kuhamisha apps au games zilizowekwa kwenye simu yako kwenda kwenye memori kadi.

Kwa msaada wa Lucky Patcher unaweza kuhamisha apps zako zilizowekwa kwenye Diski ujazo (Internal Storage) kwa urahisi zaidi. Hata hivyo ili utumie Lucky Patcher lazima simu yako iwe rooted bila hivyo hutaweza hata ku-install Lucky Patcher.

Mara baada ya kufanikiwa kwa ufanisi kuweka Lucky Patcher kwenye kifaa chako (rooted devices)  kuhamishia app ama game katika memori kadi ni rahisi. Fuata hatua hizi:

  • Hakikisha simu unayotaka kuhamisha apps zako imekuwa “rooted” na umeweka app ya Lucky Patcher.
  • Mara baada ya kuthibitishwa, fungua app ya Lucky Patcher.
  • Ikifunguka, bofya jina la app au game unayotaka kuihamishia kwenye memori kadi.
  • Mara baada ya kuchagua app ama game unayotaka kuhamisha, utaona sehemu imeandikwa “Move to /sdcard” bonyeza chaguo hilo.

  • Mara baada ya uhamisho kukamilika, itakufahamisha kuwa uhamisho umekamilishwa kwa ufanisi.
  • Bonya OK kurudi kwenye ukurasa wa mwanzo ili kuhamishia app au games nyingine kwenye memori kadi.

Kumbuka: Kwa kutumia app ya Lucky Patcher, utaweza kuhamisha programu mojamoja tu.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA