Sambaza:

Kwa nini unahitaji kugawa partition mpya katika Windows?

Diski kuu “Hard disk drive (HDD)” inaweza kugawanywa katika sehemu (partition) nyingi tofauti. Sehemu zote zinafanya kazi tofauti, hivyo unaweza kusakinisha mfumo mwingine wa uendeshaji (OS) pamoja na Windows au kuhifadhi aina tofauti za data.

Sikushauri kuweka data zako, programu, na mfumo wa uendeshaji (OS) kwenye mkasama moja (partition), kwa sababu ni kama kuweka mayai yote katika kikapu na kuongeza hatari ya kupoteza data. Ikiwa uharibifu umetokea kwenye Windows yako, data zote zilizomo kwenye mkasama wa mfumo (system partition) zinaweza kuharibiwa. Wakati wa kugawa Diski kuu, mara nyingi inapendeza kugawa partitions nyingi kwa matumizi tofauti. Mfano wa kawaida ni kugawanya Diski kuu katika sehemu 4, moja kwajili ya mfumo, na nyingine kwajili ya programu, data, na backup.

Jinsi ya Kugawa Mkasama (partition) Kwenye Windows Disk Management

Windows moja kwa moja zinakuja na mfumo wa Disk Management, ambao unaweza kutumika kutengeneza partitions mpya.

Kugawa partition mpya kwenye kompyuta yako fata hatua hizi:

  • Fungua Disk Management. Unaweza kubofya “right click”  kwenye My Computer, na kisha nenda kwenye Manage > Storage > Disk Management ili kuifungua.

  • Right click kwenye partition unayotaka kuitumia kutengeneza partition mpya na chagua “Shrink Volume”. Kisha ingiza kiasi cha nafasi unayotaka kuipunguza  na bofya “Shrink” ili kuendelea mbele.
  • Right click nafasi isiyo na sehemu (unallocated space) na uchague “New Simple Volume”. Kisha fuata hatua zinazoendelea kuunda partition mpya.
SOMA NA HII:  Jinsi ya Kufurahia Zaidi Michezo ya Kubahatisha "Kubeti"

partition
Ikiwa mtindo wa disk yako ni MBR, wakati mwingine kuunda partitions kwenye Windows 7 inaweza kushindikana na kutoa ujumbe huu “you cannot create a new volume in this unallocated space because the disk already contains maximum number of partitions” au “the operation you selected will convert the selected basic disk(s) to dynamic disk(s)“. Hii hutokea kwa sababu disk ya MBR inaweza kuwa na sehemu 4 tu za msingi (4 primary partitions). Suluhisho ni ama kubadili MBR kuwa diski ya  GPT au kutumia programu ya AOMEI Partition Assistant Standard ili kugawa partition.

AOMEI Partition Assistant Standard, ni programu ya bure kwajili ya Windows 10 / 8.1 / 8/7 / XP / Vista, inakuwezesha kugawa partition kwenye Windows katika njia nyingi. Ni njia rahisi zaidi. Bonyeza hapa kujua jinsi inavyofanya kazi.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako