Programu

Jinsi ya Kugawa Partition Kwenye Kompyuta Kwa Kutumia Programu Maalum

on

Wakati mwingine kugawa partition kwenye kompyuta kwa kutumia njia ya kawaida inaweza kushindikana kutokana na aina ya disk unayotumia au mfumo wa uendeshaji unaotumia kwenye kompyuta yako.

Kwa mfano watumiaji wa windows Xp hawawezi kutumia njia ya kawaida kufanya partition kwa sababu mfumo wa XP hauna Disk Management hivyo inakulazimu kutumia programu maalum kufanya hivyo.

AOMEI Partition Assistant Standard, ni programu ya bure kwajili ya Windows 10 / 8.1 / 8/7 / XP / Vista, inakuwezesha kugawa partition kwenye Windows kwa njia nyingi. Ni njia rahisi zaidi. Hebu tuone jinsi inavyofanya kazi:

Kwanza, weka programu hii ya disk partition na kisha ifungue.

Pili, right click sehemu ambayo ina nafasi ya kutosha ili kuunda partition mpya na chagua “Create Partition”.

Tatu, kwenye skrini hii, kokota (drag) slider ili kurekebisha ukubwa wa partition. Kisha bofya Advanced ili kubadilisha drive letter, chagua mfumo wa faili (file system), na utengeneze kama sehemu ya msingi (primary partition) au ugawaji wa mantiki (logical partition). Mfumo wa faili wa NTFS uligunduliwa na Microsoft, hivyo Windows pekee ndio inaweza kutumia mfumo huu wa faili. Ikiwa unataka kutumia partition hii kwajili ya kusanikisha Linux au mifumo mingine, ni vizuri kuchagua FAT 32. Vinginevyo, unatakiwa kubadilisha FAT32.

SOMA NA HII:  Jinsi Data Zinavyohifadhiwa kwenye Diski Kuu na Umuhimu wa Kufanya Defragmentation

Nne, baada ya kubonyeza OK, unaweza kuhakiki shughuli nzima. Ikiwa hakuna tatizo, bofya Apply ili kufanya mabadiliko. Kumbuka kuwa programu hii haifanyi mabadiliko yoyote kwenye diski yako mpaka ubonyeza chaguo la Apply.

Toa maoni yako kuhusu utendaji wa programu hii na pia usisite kutuandikia unapokutana na tatizo lolote kwenye kutumia programu hii.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.