Je Kufuta Akaunti yako ya Facebook ndio Suluhisho? #DeleteFacebook


Baada ya kampuni moja yenye makao yake jijini London, Cambridge Analytica,  kutuhumiwa kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa kijamii wa Facebook, ili kuingilia uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2016 nchini Marekani. Kampeni maalum ya kushawishi watu kufuta akaunti zao za Facebook imeanza kuwa na nguvu mtandaoni.

Kampeni hiyo ya #DeleteFacebook iliyoanzishwa na mwanzilishi mwenza wa WhatsApp, Bw. Brian Acton imezidi kushawishi watu baada ya taarifa kuhusu Cambridge Analytica kutumia taarifa za watu kutoka Facebook.


Kitendo cha Cambridge Analytica kututumia taarifa za watu kutoka Facebook kimefanya mamlaka mbalimbali za nchini Uingereza na Marekani kuchunguza iwapo taarifa za watu kutoka mataifa hayo mawili nazo zilichukuliwa bila idhini kutoka kwa wahusika.

Nako nchini Kenya, Upinzani nchini humo umetaka Kampeni za mwaka jana za uchaguzi zifanyiwe uchunguzi baada ya Cambridge Analytica kusema kuwa zimeshiriki kuwa sehemu muhimu ya ushindi mara mbili wa Rais Uhuru Kenyata.

Upinzani nchini Kenya unataka ufanyie uchunguzi kile wanachodai kuwa Kampeni za kubadilisha matakwa ya raia wa Kenya.

Je, unafikiri ukifuta akaunti yako ya Facebook ndio itakuwa suluhisho la taaarifa za watu kutumiwa bila idhini? Toa maoni yako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA