Jinsi ya kuficha (hide) picha kwenye simu za android


Hakuna mtu anataka kuharibu heshima aliyoijengwa kwa miaka mingi. Ni bahati mbaya sana kwa sekunde chache heshima yako inaweza kupotea. Kama vile sifa ya mtu ilivyo muhimu, ndivyo ilivyo picha ambazo zimo kwenye simu zake za mkononi ; na ndio sababu inatakiwa  kujifunza jinsi ya kulinda au tusema jinsi ya kuficha (hide) picha kwenye simu yako ya android.

kuficha

Fikiria hali hii:

Mpo nyumbani wewe na familia yako

Simu yako imechukilia mikononi mwako na binamu yako mwenye miaka 10, katika kubonyeza bonyeza akafungua sehemu ya picha na kukutana na picha za ajabu

Mungu wangu!!
Wakati huo, unatamani ungekuwa umefuta picha hizo maalum ulizochukua ukiwa ufukweni. Lakini umeshachelewa sana.

Heshima yako_ na akili zake_ zimeharibiwa.

Lakini kabla ya kujikuta kwenye hali kama hiyo hapo juu, ni bora kujifunza jinsi ya kujificha picha kwenye simu yako ya android, ASAP. Tuna hatua rahisi za kuzifanya mwenyewwe juu ya jinsi ya kujificha picha kwenye simu yako ya android.

[irp]

Tumia Apps zinazoficha Picha

picha kwa hisani ya:play.google.com

Kupata app kufanya kazi hiyo sio  jambo kubwa, lakini usalama wa juu wa app hiyo ni muhimu. Ni app chache sana kati ya app nyingi zina sifa kama vile: : Built-in pass-codes, Stealth modes na multiple Vaults ambazo ni njia za kusaidia kuweka picha salama. Wakati baadhi ya app hizo zinalipwa, unaweza pia kupata app za bure kwenye Hifadhi ya Google Play.

Lakini, ikiwa unataka kujua jinsi ya kuficha picha kwenye simu yako ya Android na kufanya hivyo mwenyewe, endelea kusoma.

Ficha Picha katika folda iliyofichwa (Hidden Folder)

Katika kesi hii, unaweza kujua jinsi ya kuficha picha zako .Bila kutumia nenosiri (password).

photo credit; ubergizmo.
 • Pakua (download)  file explorer, kama vile ES File Explorer, File Expert au OI FILE MANAGER.
 • Fungua file explorer yako
 • Ongeza folda jipya linaloanza na (.) ikifatiwa na jina, eg “.Party picz”.
 • Kisha chagua picha unazotaka kuzificha na ziweke picha hizo kwenye folda hilo.

Huwezi kuziona picha hizi kwenye photo gallery ,unaweza kuziona kwenye folda hii iliyofichwa tu.

[irp]

Ficha folda ya siri (Hidden Folder)

Ndio unaweza pia kujificha folda iliyofichwa (Hidden Folder) isionekane kwenye faili zako. Kufanya hivyo, fuata hatua hizi rahisi :

photo credit: ubergizmo.com
 • Gonga kwenye orodha kuu (main menu)  kwenye kona ya kushoto ya juu.
 • Bonyeza ” Settings” chini kabisa
 • Kisha gonga “Display settings”
 • Unchecked ” Show Hidden Files”. Ili kuona picha ambazo zimefichwa ndani ya file manager, unatakiwa ku-unchecked sanduku la “Show hidden files” .

Mpaka hapo utakuwa umeweza kuficha picha zako lakini kama unataka usalama zaidi, unatakiwa kutumia nenosiri (password) kuficha na kulinda picha zako. Unataka kujifunza zaidi ? nakuomba uendelee kusoma.

[irp]

Kulinda na Nenosiri
Matumizi ya third-party tools hukuwezesha kutumia nenosiri kulinda picha zako, ikiwa haitoshi kuficha picha zako kwenye hidden folder tu. Tunapendekeza app ya bure, Vaulty.

photo credit: ubergizmo.com
 • Download Vaulty
 • Installna kisha ifungue App
 • Ingiza PIN au Password unayotaka kutumia kwenye app hii.
 • Kisha bonyeza ” Hide Pictures & Videos.”
 • Chagua picha unazotaka ku-hide/lock
 • Ukimaliza bonyeza “Pad Lock”

Kufungua faili tena ni rahisi,

 • Fungua App tena
 • Ingiza PIN au Password zinazotakiwa.
 • Hapo kila kitu tayari, kazi ni kwako
photo credit: ubergizmo.com

USALAMA WA KUTOSHA
Sasa hata ukidondosha simu yako , ama ukiisahau kwenye meza nyumbani au hata kuiacha sebuleni. Unakuwa na uhakika , kwa sababu picha zako sasa zipo salama kabisa.

Ikiwa umegundua njia nyingine  ya jinsi ya kuficha picha kwenye simu za android, tuambie hapa chini katika maoni.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA