Jinsi ya kuangalia movie na TV shows kwenye simu ya Android bure


Shukrani kwa teknolojia sasa tunaweza kufurahia kuangalia movie na maonyesho mengine ya TV katika simu janja zetu bure kabisa. Hakuna haja ya kukaa mbele ya TV ili kuangalia vipindi vya televisheni au movie. Badala yake install moja ya streaming apps kwenye simu yako na uangalie maudhui unayotaka. Programu za Streaming zinapatikana kwa kwajili ya, Android na iOS. Hata hivyo, hapa katika makala hii, tutaweka baadhi ya programu bora za kuangalia movie na vipindi vya televisheni kwenye Android. Wakati baadhi ya programu zilizotajwa hapa zinalipwa nyingi ni bure kabisa.

App 10 Bora za Android Kwaajili Kuangalia Movie & TV shows

Showbox

Hii ni moja ya programu bora za kuangalia movie kwenye android imekuwa ikitumiwa na idadi kubwa ya watumiaji. Showbox streaming app ni bure kabisa kuitumia, hivyo hakuna haja ya kutumia fedha zako, zaidi ya kupakua programu hii na itawawezesha kufurahia movie pamoja na vipindi mbalimbali vya TV kwenye kifaa chako cha Android. Mara baada ya kuweka programu hii kwenye kifaa cha Android, itawawezesha kuangalia movie mbalimbali na maonyesho ya televisheni unaweza kupakua au kuangalia chochote unachotaka.

Hata hivyo, streaming app hii haipatikani kwenye Play Store, inatakiwa utembelea tovuti yao rasmi ili kuipate.

Pakua Showbox

SnagFilms

SnagFilms ni app nzuri na moja ya programu bora za kuangalia movie kwenye Android. Inaruhusu watumiaji kufurahia movie katika kila aina ya simu. Wakati SnagFilm inakuwezesha kuangalia movie kwenye kifaa chako cha Android, pia unaweza kushirikisha mapendekezo ya filamu kwenye  mitandao ya kijamii. Sehemu nyingine nzuri zaidi kuhusu streaming app hii ni kuwa inakurahisishia kutafuta movie kwa sababu  movie zimeorodheshwa katika makundi kadhaa kama vile zilizo ongezwa hivi hivi karibuni, movie maarufu na sehemu nyingine. Programu hii pia ni bure kabisa.

Pakua SnagFilms

Terrarium TV app

Unataka kufurahia movie za HD kwenye kifaa chako cha Android bure kabisa? basi bila shaka programu hii ni chaguo bora zaidi sio tu kwa movie zenye ubora pia inakuwezesha kuangalia maonyesho ya TV kwenye simu yako ya Android. Ikiwa hufurahi ufanyaji kazi wa Showbox streaming app, basi hii ndiyo chaguo bora ambayo ina msaada wa subtitle pia. Mchakato wa ku-install programu hii unahusisha hatua rahisi za haraka. Hata hivyo, hakikisha kifaa chako kina VPN ili kukuwezesha kutumia Terrarium app.

Pakua Terrarium TV

Kodi

Kodi , pengine ni chaguo bora zaidi ikiwa unatafuta programu bora za kuangalia vipindi vya TV kwenye Android pamoja na movie. Sio tu kwa maonyesho ya televisheni au movie badala ya unaweza kufurahia muziki, michezo, na viral videos pia kupitia programu hii. Hii ni programu ya bure kabisa, tena hakuna haja ya kutumia fedha zako. Mchakato wa ku-install kidogo kuchukua muda, hivyo uwe tayari kujitolea kiasi kidogo cha muda unaohitajika kuanzisha Kodi kwenye simu yako Android.

Pakua Kodi

Videomix


Videomix ni moja ya programu za zamani sana za Android zinazokuwezesha kuangalia vipindi vya televisheni bila malipo. Unaweza kufurahia movie kupitia programu hii.Movie kwenye app hii  zimepangwa kwa kufuata mwaka, aina na nchi ya uzalishaji. Programu hii inasasishwa mara kwa mara ili kuhakikisha filamu zote mpya na maonyesho ya TV ya hivi karibuni yanapatikana katika programu hii.

Pakua Videomix

MovieHD


Jina lake linaonyesha kuwa programu hii inaonyesha maudhui ya HD iwe ni filamu au TV shows haijalishi. Programu hii inafanya kazi kikamilifu kwenye vifaa vya Android na iOS. Kitu kizuri ni kuwa, programu hii pia ni bure kabisa.

Pakua MovieHD

Viewstar

Nyingine kwenye orodha ya programu bora za kuangalia filamu na vipindi vya televisheni kwenye Android. Programu hii ni bure kabisa na haihitaji usajili wowote au malipo ili kupata filamu kutoka Viewstar. Wale wanaopenda kutazama anime, programu hii ni tiba kamili kwao kwa sababu maudhui yake makuu ni anime. Kwa hiyo, ikiwa unatafuta series mpya za Kijapani au aina ya kawaida ya anime, programu hii inakupa kila kitu.  Programu hii inapatikana kwenye duka la Google Play, hata hivyo, unaweza kuipata kwenye tovuti rasmi pia.

Pakua Viewstar

PlayView


PlayView bila shaka ni streaming app nzuri kutajwa katika orodha hii ambayo ni bure kabisa kuangalia maonyesho ya TV na filamu kwenye Android. Kipengele kimoja cha kipekee kwenye programu hii ni kukuwezesha kuchagua “stream quality”.

Pakua PlayView

Popcorn Flix

Ingawa jina lake ni linafanana sana na Netflix, ni programu tofauti kabisa ambayo unaweza kuangalia movie mbalimbali bila malipo. Kwa mujibu wa madai yao, movie mpya zimeongezwa kila siku, hivyo utakuwa na machaguo wakati unatafuta filamu bora ya kutazama.

Pakua Popcorn Flix
 

Kwa hiyo, hizo ni programu bora za kuangalia movie na vipindi vya televisheni kwenye kifaa chako cha Android. Programu nyingi ambazo tumeziorodhesha hapa ni bure, kwa hiyo unaweza kuziweka  kwenye simu janja yako na kufurahia burudani zaidi.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA