Sambaza:

Katika kuhakikisha ajenda ya viwanda inafikiwa, Global Education Link Limited (GEL) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Lovely Professional cha India wataanza kutoa kozi fupi za masomo ya maendeleo ya viwanda.

Kwa mujibu wa GEL kozi hizo fupi zinalenga kuziba mapungufu yanayohitajika kwenye ajenda ya maendeleo ya viwanda.

Akizungumza  leo (Alhamisi) katika maonyesho ya biashara ya Kimataifa ya 41 yanayoendelea jijini Dar es Salaam , Meneja mradi Medard Sotta amesema uchumi wa viwanda unategemea wafanyakazi ambao wataendesha mashine na teknolojia, ili kiwanda kiendeshwe vizuri kinahitaji wafanyakazi wenye ujuzi wa kutosha.

Amefafanua kwa kulitambua hilo kampuni yao imeamua kuwekeza kwenye mafunzo ya muda mfupi yatakayosaidia kuzalisha wafanyakazi kwenye ujuzi watakaosaudia uchumi wa viwanda kufikiwa kwa haraka.
Amesema hivi karibuni GEL na chuo hicho watasaini makubaliano ili wanafunzi waanze kuomba usaili kwa ajili ya hizo kozi fupi.

“Lengo kuu ni kuwaunganisha wanafunzi wa ndani na wa nje pia tunataka kuisaidia Serikali kufikia mafanikio chanya kwenye ajenda ya viwanda ikiwamo hii ya kutoa kozi fupi.

Sotta aliongeza kampuni yake itaendelea kusaidia wanafunzi wanaosoma katika vyuo vikuu nje ya nchi wanaotambuliwa na TCU.

GEL imesaifia wanafunzi wapatao 500 kupata nafasi za masomo katika nchi mbalimbali za nje kuanzia mwaka 2006 wengi wao wakiwa wanachukua masomo ya Afya.

SOMA NA HII:  Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

Katika nyanja nyingine kampuni hiyo inafanya majadiliano kati ya Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) na Chuo Kikuu Shenyang Aerospace cha China ili waanze kubadilisha programu za masomo.

Amesema wanafunzi ambao wanachukua kozi za miaka minne kupitia mpango huo wanaweza kusoma miaka miwili Tanzania na miwili nchini China.

Maonyesho ya biashara ya kimataifa yaliyoanza Juni 28 na yatamalizika Julai nane mwaka huu yakiwa na kauli mbiu “Ukuaji wa biashara kwa maendeleo ya viwanda”.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage alisema maonyesho ya mwaka huu yanalenga kusaidia wajasiriamali wadogo wadogo kuingia katika uchumi wa viwanda.

Amesema maonyesho hayo yanahusisha kampuni kutoka nchi 30 mbalimbali na kampuni 2,500 zinashiriki kuonyesha bidhaa zao.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako