Apple iOSIntaneti

Muda ambao Korea ya Kaskazini imetoa Tablet na kuiita “iPad” & Apple hawawezi kufanya lolote

Kampuni moja ya kiteknolojia kutoka Korea Kaskazini—Myohhang— wamezindua “Tablet” mpya ambayo imepewa jina la iPad ambayo ni chapa maarufu ya kampuni ya Apple na kufanya kuwa kifaa cha kwanza kilichotengenezwa Korea ya Kaskazini na kutumia chapa ya Apple.

Ryonghung iPad imetengenezwa kuwawezesha watumiaji kusoma habari, kufanya kazi kwenye nyaraka mbalimbali na kutumia zaidi ya Apps 40 ambazo tayari zimewekwa, ikiwa ni pamoja na moja ambayo inaweza kutambua maradhi 1,200 na kupendekeza tiba.

Inawezeshwa na quad-core 1.2GHz CPU na inakuja na 1GB ya RAM na uwezo wa kuhifadhi wa 8GB.


Sasa, kwa mujibu wa hati miliki ya biashara huu ni muongozo wa Apple:

‘You may not use or register, in whole or in part, Apple, iPod, iTunes, Macintosh, iMac, or any other Apple trademark,’ the guidelines state, ‘including Apple-owned graphic symbols, logos, icons, or an alteration thereof, as or as part of a company name, trade name, product name, or service name except as specifically noted in these guidelines.’

Lakini Korea ya Kaskazini haijali lolote ?

Ukweli ni kwamba, Apple hawawezi kuipeleka kampuni hii mahakamani kwa sababu Korea ya Kaskazini ipo kwenye dunia ya peke yake.
Binafsi, mimi sidhani kama walitakiwa kuiita tablet kwa sababu inaonekana kama laptop ya mtoto ?

SOMA NA HII:  Google Sasa Kuzuia Matangazo Kupitia Kisakuzi Kipya cha Chrome

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako