Kompyuta

Kompyuta yenye siri za rais wa Marekani yaibwa

on

Kompyuta ya kikosi cha kumlinda rais wa Marekani inayoripotiwa kuwa na michoro ya jumba la Trump Tower, na taarifa zingine za siri imeibwa kutoka kwa gari la afisa mmoja mjini New York.

 Kompyuta yenye siri ya kikosi cha kumlinda rais wa Marekani yaibwa

Kompyuta yenye siri ya kikosi cha kumlinda rais wa Marekani yaibwa

Hata hivyo kikosi hicho cha kumlinda rais kinasema kuwa kompyuta hiyo haikuwa na taarifa za siri.

Lakini wanasema kuwa ina taarifa kuhusu uchunguzi wa aliyekuwa mgomea wa Democratic Hillary Clinton kutumia barua pepe ya kibinafsi.

Kwa sasa polisi wanachunguza kamera za siri kuweza kumtambua mshukiwa.

Shirika la ABC lilisema kwa gari la ajenti lililengwa katika eneo la Bath Beach kwenye mtaa wa Brooklyn.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuzuia "Automatic Updates" Kwenye Windows 10

CBS nayo ilisema kuwa kampyuta hiyo ilikuwa na taarifa muhimu kumhusu Papa Francis

Taarifa za polisi zililiambia gazeti la The York Daily News, kuwa taarifa zilizo kwenye kompyuta hiyo ni za siri kubwa.

Kompyuta hiyo inaripotiwa kuibwa kutoka kwa mkoba uliokuwa ndani ya gari. Mkoba huo hata hivyo umepatikana lakini kompyuta yenyewe bado inatafutwa.

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Reply

Your email address will not be published.