Kompyuta

Kompyuta Ni Nini? Fahamu Aina Za Kompyuta Na Kazi Zake

Tarakilishi au Kompyuta ni mashine au chombo cha kielektroniki chenye uwezo wa kupokea na kukusanya taarifa (data), na kuzifanyia kazi kulingana na kanuni za programu inayopewa kwa kufuata hatua za kimantiki katika ufanyaji wa kazi. Hutoa matokeo ya kazi hiyo na namna ilivyoendeshwa, pamoja na kutoa matokeo ya kitu kilichofanyika, yaani kinachoonekana (Information) kwa haraka.

Kompyuta Ni Nini? Fahamu Aina Za Kompyuta Na Kazi Zake

Teknolojia hii ni mabadiliko ya kisayansi yaliyowekwa kwenye nadharia ya utendaji kazi. Mabadiliko hayo yanapochochewa kwa kiasi kikubwa huwezesha mambo mbalimbali kuvumbuliwa na kuweza kuboresha shughuli mbalimbali za kijamii, kiuchumi na hata mawasiliano.

Kompyuta ni moja kati ya nyenzo zilizotokana na mabadiliko ya teknolojia ya hali ya juu.

Aina za kompyuta

Wengi wanaposikia kompyuta huelekeza mawazo yao kwenye kompyuta za mezani (Desktop Computers) au kompyuta mpakato (Laptop Computers), lakini ukweli ni kwamba kuna aina nyingi za kompyuta zaidi ya hizo mbili nilizokwisha zitaja hapa. Na kwa maendeleo ya tekinolojia yalipofikia hivi sasa, ni muhimu ukafahamu kuwa kompyuta zimetuzunguka kila mahali, ziko mezani, mikononi, barabarani, hospitali, na kila mahali.

Kimsingi kompyuta zimegawanyika katika aina kuu tatu , nazo ni kama ifuatavyo:-

1. Digital Computers:
Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kufanyia hesabu pamoja na kazi za kutumia akili. Kompyuta za aina hii ndio ambazo zipo katika matumizi hasa katika Dunia hii ya mabadiliko ya teknolojia.

SOMA NA HII:  Jinsi Data Zinavyohifadhiwa kwenye Diski Kuu na Umuhimu wa Kufanya Defragmentation

2. Analog Computers:
Ni kompyuta zinazotumika kwa ajili ya kupokea taarifa (Data) kama zile za kusomea hali ya hewa, kupimia mishipa ya damu na kupimia kiwango cha chumvi kwenye maji.

3. Hybrid Computers:
Kompyuta hizi zinafanana na zile zilizotangulia kutajwa hapo mwanzo, nazo zinatumika kwa ajili ya kutafutia taarifa (Data) kutoka kwa binadamu moja kwa moja na kupitia mandishi na vipimo.

Tarakilishi(kompyuta) zinaweza kuainishwa kulingana na Ukubwa wa umbo, Dhumuni, na Utendaji kazi.

Aina za digital kompyuta

 • Tarakilishikuu (Super Computers):

Tarakilishi hii inashughulikia kiwango kikubwa cha hesabu za sayansi na inahifadhiwa katika chumba chenye mfumo poza maalum ambao unaunganisha uyoyozwaji hewa na kimiminiko poza ili kupunguza joto.

kompyuta Blue Gene/P iliyopo Maabara ya Kitaifa ya Argonne
Tarakilishikuu Blue Gene/P iliyopo Maabara ya Kitaifa ya Argonne

Tarakilishikuu inachukua nafasi muhimu katika sayansi ya mahesabu, na zinatumika kwa mapana kwenye kazi makini za mahesabu katika nyanja mbalimbali, ikiwa ni pamoja na utabiri wa hali ya hewa, tafiti za tabia nchi, chunguzi za mafuta na gesi, ukokotozi wa maumbile na tabia za michanganyiko ya kemikali, kazi za kijeshi na sehemu za ukaguzi.

 • Tarakilishi kiunzikuu (Mainframe Computers):

Tarakilishi kiunzikuu ni tarakilishi ambazo kimsingi zinatumiwa na kampuni na mashirika ya serikali kwa matumizi makinifu, kuchakata data nyingi kama vile sensa, takwimu za viwanda na biashara, upangaji rasilimali za kazi, na uchakatuaji mali.

Ndani ya kompyuta
Ndani ya Tarakilishi kiunzikuu IBM System Z9

Tarakilishi kiunzikuu pia inajulikana kama “Big Iron” ni ndogo na haina nguvu sana kama Tarakilishikuu katika uwezo wa ukokotoaji. Inahusika na utunzaji wa faili na kumbukumbu kubwa sana.

 • Mini Computers:
SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuongeza Nafasi Kwenye Kompyuta

Aina hizi za kompyuta zilidhihiri katika kipindi cha miaka ya sitini.Ni kompyuta zenye umbile dogo kuliko zile zilizotangulia kutajwa,na ni bora kwa kuunganishia kompyuta nyengine zinazotumika viwandani na ndani ya nchi.

 • Micro Computers:

Aina hii ya kompyuta inakusanya aina zifuatazo:-
Personal Computers (PCs) ambazo ni maalumu kwa ajili ya matumizi ya mtu mmoja tu. Home Computers, Portable Computers: Nazo ni kompyuta za kubeba mkononi, ambazo zimegawanyika katika aina zifuatazo:

 • 1. Laptop.
 • 2. Notebook.
 • 3. Palmtop.
Kazi za msingi za kompyuta
 1. Kazi za uingizaji (Input).
 2. Kazi za uwendeshaji au ufanyishaji (Proccessing).
 3. Kazi za utoaji (Output).
 4. Kazi za kuhifadhi (Storage)

Hitimisho

Tumejifunza kompyuta ni nini?, na watu hutumia kompyuta kufanya mambo gani, pia tumeona baadhi ya aina mbali mbali za kompyuta na kufahamu matumizi yake na mipaka yake kwa ujumla.

Somo hili halitaishia hapa kwani bado kuna mengi ya kujifunza kuhusu kompyuta hizi, kwenye makala nyingine tutajifunza kuhusu matumizi ya Kompyuta na sifa za programu endeshi za kompyuta hizo.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku, Karibu Kwa Pamoja Tujenge Jamii Ya Wanateknolojia!.

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako