Nyingine

Kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi atimuliwa

Baada ya kudumu kwa takriban miaka miwili, kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Danny Blind hatimaye ametimuliwa kufuatia muendelezo wa matokeo mabaya kunako timu hiyo.

Hii inafuatia kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Bulgaria siku ya Jumamosi na kuwaacha Uholanzi katika nafasi ya nne kwenye mbio za kufuzu kushiriki kombe la dunia 2018 Russia.

Blind mwenye miaka 55 ambaye alichukua nafasi ya kuifundisha timu hiyo kutoka kwa Guus Hiddink mwaka 2015, lakini akashindwa kuipeleka kwenye michuano ya Euro Ufaransa mwaka jana.

Mholanzi huyo amepoteza mechi 5 kati ya 9 za ushindani ambazo ameiongoza Uholanzi tangu apewe kibarua hicho mwaka 2015.

Kipa wa zamani wa Ajax Fred Grim ndiye aliyeteuliwa kuwa kocha wa muda wa timu hiyo na ataiongoza kesho jumanne kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Italia.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuepuka Makosa 5 Yanayofanywa na Wamiliki wa Website

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako