Kitu Gani Natakiwa Kufahamu Kuhusu Muonekano “UI” Mpya Ya Windows 8?


Swali: Ninahitaji kujua nini kuhusu UI ya Windows 8?

Labda mabadiliko makubwa ambayo Microsoft imefanya kwenye mfumo wa uendeshaji (operating system) wa Windows 8 ni ushirikiano wa user-interface mpya kabisa. Watumiaji wa mifumo ya uendeshaji ya Windows ya awali wanaweza kujikuta wamechanganyikiwa kutokana na kukosekana kwa “Start menu” na programu mpya ambazo hazina kifungo (button) nyekundu cha “X”. Tumeandika orodha ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara ili kuwasaidia watumiaji kutumia vyema mfumo mpya wa Microsoft.

Kitu Gani Natakiwa Kufahamu Kuhusu Muonekano "UI" Mpya Ya Windows 8?-mediahuru

Jibu:

Haiitwi tena Metro.

Wakati Windows 8 ilipotolewa kwa mara ya kwanza kwa umma mwaka 2011, Microsoft iliunda interface mpya rafiki ya kugusa “Metro.” Kutokana na matatizo ya masuala ya alama za biashara na kampuni kutoka Ujerumani, Microsoft sasa wameachana na jina hilo kwa kuiita Windows UI mpya ya au Windows 8 UI.

Hakuna tena orodha ya Mwanzo (Start menu).

Badala ya kutumia menu interface kufikia programu, Windows 8 imehamia kwenye “graphical tile display”. Unaweza kufikia “Start screen display” mpya kwa kubofya kwenye kona ya chini ya kushoto ya desktop yako ambapo ulitarajia kuwe na kifungo cha Mwanzo (start button). Windows 8 imeunda viungo (links) vya mstatili kwa programu zako inayojulikana kama “tiles”. Ikiwa kuna programu umeinstall lakini hauioni tile kwajili yake, unaweza kubonyeza right-click kwenye skrini ya Mwanzo (Start screen) na kisha bofya “All Apps” ili uone kila kitu kilichowekwa kwenye kompyuta yako. Mwonekano ambao unajumuisha vitu vyote unaweza kuwa na mvuto zaidi kwako .

SOMA NA HII:  Jinsi ya kubadili mpangilio wa keyboard ya kompyuta kuwa Dvorak keyboard

Programu zako za kawaida bado zinafanya kazi.

Wakati Microsoft inatangaza zaidi programu mpya za kusisimua za Windows 8 , toleo kamili la mfumo wa uendeshaji (operating system) inawezesha programu nyingi ambazo unaweza kutumia na Windows 7. Ingawa toleo la Windows 8 linalojulikana kama Windows RT, ambayo inaendeshwa kwenye vifaa vya simu pekee, inawataka watumiaji wake kutumia programu za Windows 8 tu.

Hifadhi ya Windows (Windows Store) ina programu zote za kisasa unazozihitaji.

Ikiwa unataka kujaribu programu mpya za Windows 8, unaweza kuzipakua kwenye Windows store. Angalia tile ya kijani kwenye Start screen iliyoandikwa Store. Unaweza kutafuta kupitia programu zilizopo na kuzipakua kwenye kifaa chako.

 Windows 8 apps hazina menus ya kawaida unayoweza kutarajia.

Kufungua programu ya Windows 8, bonyeza tu au gusa tile yake kwenye skrini ya Mwanzo (Start screen). Programu hizi daima huwa skrini kamili na hazina kitufe cha menyu (menu buttons) unayotumia kufunga programu kwenye desktop. Kufunga programu ya Windows 8 unaweza kuiondoa (tazama hapa chini), unaweza kubofya sehemu ya juu ya window na kuipeleka chini ya skrini, au unaweza kuright-click-au kubofya kwa muda mrefu kwenye menyu ya kivinjari (switcher menu) na kisha bofya close. Bila shaka, unaweza pia kuifunga kwenye Task Manager.

 Utahitaji kutumia pembe nne za Windows 8.

Ikiwa haujawahi kusikia pembe nne za Windows 8 (four-corners of Windows 8), utaona zimetajwa wakati unapoanzisha kufanya setup ya Windows 8 OS yako. Hii inamaana kwamba katika Windows 8, kuweka mshale wako katika moja ya pembe nne za skrini yako itafungua kitu.

    • Chini au Juu-kulia – Kuweka mshale wako katika moja ya pembe za kulia kunafungua Charms menu. Orodha hii hutoa viungo (links) za zana na huduma (tools and utilities) ambazo utatumia mara kwa mara kama mipangilio ya programu (app settings), mipangilio ya PC (PC settings), na search charm.
    • Chini-upande wa kushoto – Kona ya chini ya kushoto inafungua link kwenye skrini ya Mwanzo (Start screen).
    • Juu-kushoto – Kona ya juu ya kushoto inafungua kiungo kwenye programu ya mwisho uliyokuwa unaitumia. Hii inaruhusu kubadili kwa urahisi kati ya programu na programu. Swipe chini kutoka kwenye kona ya juu kushoto ili kufungua Switcher menu inayoonyesha programu zote ulizofungua. Unaweza kuchagua programu kutoka kwenye orodha ili kuitumia kwa muda huo.
SOMA NA HII:  Je Kuna Programu ya Windows Unatamani Kuitumia Kwenye Simu ya Adroid ?

Ingawa imekuwa optimized kwajili ya kugusa (touch), Windows 8 UI inafanya kazi vizuri na keyboard na mouse.

Ingawa UI Windows 8 inafaa zaidi katika mazingira ya kugusa (touch-enabled), bado inafanya kazi vizuri kwenye desktop au laptop na mouse au trackpad.

Lock screen inaweza kuwachanganya watumiaji wa desktop.

Ikiwa unachanganyikiwa unapojaribu kuingia kwenye akaunti yako kwa sababu huoni mahali pa kuingia neno lako la siri (password) au kuchagua akaunti yako ya mtumiaji, usijali.

Windows 8 hutumia lock screen ambayo inaonyesha background ya kipekee na “configurable notifications” wakati akaunti yako imefungwa. Bonyeza kitufe chochote kwenye kibodi yako na lock screen itapanda juu na kuonyesha uwanja wa neno la siri la akaunti yako.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA