Kirusi Kipya “ATMii Malware” Kinaweza Kutoa Pesa Zote Kwenye ATM


Sifa ya ATM kupoteza fedha ni sifa mbaya zaidi kwa benki, lakini watafiti wa Kaspersky Lab wamegundua virus (malware) mpya zinazofanya hivyo. Inalenga mashine za ATM, ina uwezo wa kuruhusu washambuliaji kutoa pesa zote zilizomo kwenye mashine ya ATM.

Inajulikana kama ATMii, malware hii ni nyepesi. Inajumuisha sehemu mbili – moduli ya injector (exe.exe), ambayo inalenga programu ya ATM inayoitwa atmapp.exe, na moduli ya kuingizwa (dll.dll). Command mbaya zinatumika kuvamia maktaba ya wamiliki halali; wahalifu wanaweza kufikia ATM husika kupitia mtandao au kwa njia ya kawaida kupitia “USB ports” ili kupakia mafaili mabaya kwenye mifumo.

SOMA NA HII:  Mambo Yaliyompa Ushindi Mmiliki wa Facebook Dhidi ya Maseneta wa Marekani

ATM

Wakati wa uchunguzi, watafiti wa usalama waligundua kuwa kirusi kina “command” zisizo salama, zilizoandikwa kupitia Visual C na zinaonyesha muda wa uongo wa miaka minne iliyopita. Malware inafanya kazi kwenye matoleo ya Windows ya hivi karibuni kuliko Windows XP, ambayo inatumiwa na mashine nyingi za ATM zinazofanya kazi kwa sasa.

Kaspersky Lab katika chapisho la blogu imesema kwamba ATMi ni mfano mwingine wa jinsi wahalifu wanavyoweza kutumia kipande kidogo cha kanuni ili kuhamishia fedha kwao. Sampuli ya ATMii Malware ilitolewa na mshirika wa Kaspersky Lab kutoka sekta ya fedha mwezi Aprili 2017; inaendana na toleo la hivi karibuni la malware za Skimer, zilizoripotiwa na Kaspersky Lab mwaka jana na ni malware za hivi karibuni za ATM.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kugundua (na kuepuka) barua pepe za udanganyifu

Ili kujilinda dhidi ya mashambulizi hayo, Kaspersky Lab inashauri waendeshaji wa ATM kuingiza sera za kukanusha na kudhibiti kifaa, pamoja na hatua za kiufundi za kulinda ATM dhidi ya upatikanaji wa moja kwa moja.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *