Makala

Kifo Cha Msanii Wa Afrika: Blogs, Free Downloads Na Takwimu

Kufanya kitu kilele kile kila siku na kutarajia matokeo tofauti unaweza kuita ni kuchanganyikiwa. Mimi naona ni kama zoezi la kupoteza muda na rasilimali. Huu ni mzunguko ambao wasanii wa Afrika wamefungwa na kuna mfumo ndani yake:

  • Kutoa albamu kwajili ya kuuza kwenye majukwaa ya kimtandao (digital platforms).
  • Ndani ya dakika chache baada ya album kutoka blog zinaaza kutoa link ya bure (na kinyume cha sheria) ya kupakua album.
  • Msanii anafahamu uharamia huo na anaanza kulaumu mashabiki na blogu kuwa hawatoi ushirikiano kwenye kazi zao.

Kwa nini wasanii bado wanashangazwa na jambo hili wakati linatokea kila siku ?

Siwezi kuelewa kuchanganyikiwa kwao, na nashangaa. Kutengeneza kazi yenye ubora inachukua masaa mengi kwajili ya maandalizi, maelfu ya pesa,na uwekezaji mkubwa wa hisia. Kitu kinachonishangaza na siwezi kuelewa au kuwa mwenye huruma ni kwa nini wasanii bado wanashangaa au wamekata tamaa kutokana na kutokea kwa jambo hili wakati wao ndio waanzilishi wa utamaduni huu wa uharamia ambapo mashabiki wanahitaji upakuaji kwa kila kitu bure.

Mwanzo

Mwanzoni mwa karne, Swala la Intaneti liliibuka. Lilikuwa jambo jipya na la ajabu ambalo liliwasilisha njia nafuu na rahisi ya kusambaza bidhaa papo kwa papo. Waafrika wanaoishi nje walikuwa wanatafuta njia ya kuungana na muziki kutoka nyumbani barani Afrika wakaangukia kwenye intaneti. Tovuti, blogu, na majukwaa ya kijamii yakageuka kuwa vyanzo mahiri kwajili ya “kushare” muziki wa Afrika.

Wanamuziki wa kizazi kipya barani Afrika hawakuweza kutumia njia za asili za matangazo au usambazaji. Kazi zao zilipotezwa kama mtoto wa Mmarekani mweusi ambaye hakuwa na nafasi katika nchi aliyozaliwa. Na kutokuwepo kwa msaada katika mwanzo wao ilipelekea wasanii hawa kupata jamii ya kuwaamini kwenye intaneti.

Kuwepo kwa Intaneti kulipelekea rapa ambaye yupo Tanzania kuwafikia wasikilizaji waliopo Canada, na jamii hizi ndogo zilijenga uhusiano na kuanza kubadilishana bidhaa. Katika miaka ya 2000, blogu za muziki na majukwaa ya jumbe mbalimbali yalikua kutoka kuwa majukwaa ya jamii na kuwa majukwaa muhimu kwa wasanii na mashabiki.

Kwa matumaini ya kutumia majukwaa haya kupata mashabiki wengi zaidi, wasanii wa Afrika walichukua uamuzi wa kuacha kuuza muziki wao kwa njia za kawaida (kanda na CD) na kuruhusu muziki wao kusambazwa bure kwenye mtandao (wakati mwingine kinyume cha sheria). Hii ni sawa na kusema “kufunga biashara”: Kutoa sadaka mapato yanayotokana na mauzo ya CD kwenye hadhira ndogo kwa ajili ya kufikia hadhira kubwa kupitia mtandao. Wasanii walikuwa na hamu ya kutafuta njia mpya na nafuu ya kusambaza kazi zao, na Intaneti ikawa mbadala kamilifu.

Kabla ya hapo, usambazaji wa muziki ulikuwa na gharama kubwa na ni mchakato ambao ulikuwa na ugumu ndani yake . Muziki ulitakiwa kurekodiwa na kuwa mastered, CD ilibidi zichomwe, na mbele na nyuma ya CD covers zilihitajika. Kwa baadhi ya wasanii, michakato hii ilikuwa na gharama kuliko uwezo wao. Baadhi ya nyimbo hazikuwa “mastered” vizuri au hazikusambazwa kupitia njia hizi kwa sababu ya gharama na kuenea kwa uharamia. Na baada ya yote hayo, CD bado zilitakiwa kusambazwa kwa mashabiki na wauzaji. Hii inamaanisha msanii alitakiwa kupanda basi na kwenda kusambaza CD kwenye masoko, vituo vya redio, Madj, na kuwafikishia mashabiki. Kwa wasanii wapya, CD hizi mara nyingi zilitolewa bure kwanza kabla ya kuweza kuuza. Kuanza kazi kwa mara ya kwanzaa ilihitaji mtaji mkubwa na hakuna dhamana kama hela zitarudi. Intaneti ilitatua tatizo hili, msanii alitakiwa kutuma wimbo wake kwa njia ya barua pepe tu kwenda kwenye tovuti. Na usambazaji ulijiendesha wenyewe.

Mashabiki kutoka pande zote za dunia waliweza kupata wimbo na kutoa maoni yao ndani ya muda mfupi bila ya kutumia gharama ambazo zilitumika kwenye njia za mwanzo za kusambaza muziki. Wasanii pia waliweza kusoma maoni ya mashabiki na kujua ni kiasi gani wimbo umekuwa maarufu kwa kungalia idadi ya “download”  na maoni. Kwa wakati ule ilionekana kama matatizo yao yote yamepata ufumbuzi, kumbe walikuwa wanatengeneza tatizo jipya.

Tatizo lililotengenezwa

Upakuaji wa bure ulikua na maana wakati muziki wa kizazi kipya barani Afrika unaanzishwa; wakati hakuna mfumo imara wa muziki. Kutoa muziki bure kamwe haikuwa ufumbuzi wa kudumu, au haipaswi kuwa.

SOMA NA HII:  Je Thamani Ya Mchezaji Inaweza Kuongezeka Kupitia Mitandao Ya Kijamii?

Kutoa kazi bure ilikuwa ni njia ya kumtambulisha msanii kwa urahisi kwenye soko, na kuruhusu muziki wake kueneza bila ya mipaka inayowekwa na mifumo ya kulipwa.

Hii ni kawaida katika masoko ya bidhaa.

Unapoenda supermarket ama unapo nunua gazeti unaweza kukutana na gazeti la bure ndani yake. Hii inamaanisha utambulisho wa bidhaa. Ijaribu na ufanye maamuzi kama unaweza kununua ama haupo tayari kutumia fedha zako kununua bidhaa hiyo hapo baadae.

Kwa Marekani na Ulaya , wasanii wapya wamegundua jinsi ya kutumia mfumo wa bure na wa kulipia kwa ufasaha zaidi. Msanii mpya anatoa wimbo bure ama hata “mixtapes/albums”, hadi atakapokuwa maarufu na kisha kuanza kuuza muziki wake kwa kuwaomba mashabiki wanunue nyimbo zake. Mala moja moja , msanii atotoa wimbo wa bure ili kuendeleza uhusika wake na kusema “Asante” kwa mashabiki. Bado wana hakikisha mala kwa mala wanatoa muziki kwaajili ya mashabiki kununua.

Mfumo huu unafanya mambo mawili muhimu sana :

  • Kwanza, Unawajenga mashabiki kuthamini muziki unaotengenezwa na msanii . Kwa kuongeza thamani kwenye kazi ya sanaa, ni dhahiri shabiki atakuwa tayari kununua muziki. Mashabiki wataanza kuelewa kuwa kuwasupport wasanii wanaowapenda inatakiwa wanunue kazi zao.
  • Pili, inampa msanii ishara za kweli za umaarufu wake. Shabiki ambaye yupo tayari kununua muziki wako ni wathamani kuliko msikilizaji wa kawaida ambaye yupo tayari kushusha kazi za bure tu. Ni rahisi kufikisha downloads 20,000 kama wasikilizaji hawatakiwi kulipia . Kuwa na ufahamu juu ya nani yupo tayari kulipia muziki wako inamsaidia msanii kujua ana mashabiki wangapi wenye thamani kubwa kwenye muziki wake. Kama wapo tayari kulipia elfu 10000 kwa ajili ya album, labda wapo tayari kununua tiketi kwajili ya tamasha lako na pengine kutumia elfu 20000 zingine kwajili ya bidhaa zako( t-shirt, kofia na nk). Aina hii ya taarifa ni muhimu kuzifahamu kwa wasanii wapya na wanaojijenga kwenye sanaa.

Wasanii wa Afrika walipuuzia hatua hii na kuendelea kutoa sehumu kubwa ya muziki wao bure, wao ndio waliotengeneza tatizo kubwa linalo wakumba hivi sasa.

Kutengenezwa kwa adui


Licha ya “message boards, forums na blogs” kuwa sehemu maarufu za kupata nyimbo mpya mwanzoni mwa miaka ya 2000, kuanzisha tovuti ilikuwa ni gharama kubwa kwa msanii na label ndogo za muziki. Gharama za kutafuta “website designer” na Internet host ya kuaminika ilikua kikwazo.

Kuingia kwa blog za muziki.

Blogs zilikuwa tayari kuingia kwenye gharama hizi kwa sababu “downloads” ziliongeza trafiki. Trafiki wengi zaidi ni sawa ni na watembeleaji wengi zaidi wa tovuti: watembeleaji wengi wa tovuti inamaanisha kuongezeka kwa njia za kutengeneza pesa kutoka kwenye matangazo; na pesa nyingi inamaanisha faidi zaidi. Faidi inaweza kutumika kuwekeza kwenye kupata sehemu kubwa zaidi kwajili ya blog kuweka nyimbo nyingi , na mzunguko unaendelea tena na tena.

Blogu za Kupakua muziki zilikuwa na umuhimu mkubwa mwanzoni mwa usambazaji wa muziki kwa njia ya mtandao kwa sababu wasanii hawakuwa na rasilimali za kuanzisha tovuti zao. Blogu zilisaidia kuwatangaza wasanii waliotuma muziki wao kwa kuwatambulisha kwa watembeleaji wa mara kwa mara wa blogu zao. Mashabiki wakajijengea tabia ya kutembelea tovuti chache ambazo zina nyimbo zote wanazohitaji , ambazo ni rahisi kupakua. Hakukua na uhitaji tena wa kujiunga na forum, kukumbuka password, na kisha kufungua mada nyingi kutafuta muziki mpya .Ulikua uhusiano wa ushindi kwa ushindi . Hata hivyo, uhusiano huu kamwe haikumaanisha uwe wa kudumu, na sasa umeanza kuzinufaisha blogu zaidi kuliko ilivyo kwa wasanii wenyewe kwa sababu kadhaa.

Madhumuni ya blogu za muziki ni kuwatangaza wasanii kwa mashabiki wapya, wanaainisha aina ya kazi zao, kutoa uchambuzi na ufafanuzi kuhusu muziki na utamaduni unaozalisha muziki. Kama blogger kila anachofanya ni kutoa “downloads link” tu, hapo hawamnufaisha msanii au msomaji zaidi ya kutengeneza mfereji wa kutoa muziki bure. Kwa sababu msanii hawezi kutoa muziki kila siku ila miziki yao inaendelea kuwepo kwenye mzunguko wa blog kila siku.

Blogu kadhaa zinazojulikana kwa kuchukua muziki kutoka kwa wasanii, (wakati mwingine kinyume cha sheria na bila idhini) na kuzitoa bure. Wimbo utaondolewa utambulisho wake wa awali “ID3 tags na artwork” na kubadilishwa na jina la blogu hiyo. Kuhakikisha unajua wapi unaweza kupakua muziki, blog pia itaongeza “blog audio tone” kwenye wimbo wako. Katika hali hiyo wasikilizaji wanaweza kupenda wimbo lakini wasijue nani aliyeimba kwa sababu blog imejitangaza kila sehemu ya kazi yako. Katika matukio mengine, wasanii wamekataa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya blogu ambazo zinaiba kazi zao kwa kuwa wanathamani idadi ya download zaidi ya kazi walizotengeneza kwa taaluma zao. Wasanii wengi wanafanya kazi chini ya dhana ya uongo kuwa idadi kubwa ya download, kisheria au vinginevyo, inasaidia katika “show bookings” na “brand endorsements”.

SOMA NA HII:  Mtandao utumike kusukuma mbele gurudumu la huduma na maendeleo

Baadhi ya blogu zinawalazimisha wasanii kulipia ili muziki wao uwekwe kwenye tovuti. Haya ni Maajabu! msanii analipia ili muziki wake uweze kusambazwa kwenye blog kinyume cha sheria hii ni aibu. Kitu kinachonishangaza zaidi ni kuona wasanii wengi wanaruhusu yote haya kutokea na kuamini hii ni njia pekee ya kuwa maarufu.

Blogu zinawahitaji wasanii. Wasanii hawazihitaji blogu.

Kwa kuruhusu tovuti ziendelee kutoa huduma ya kupakua muziki bure ,wasanii wanafanya mashabiki wao wazithamini zaidi blogu kuliko wasanii wenyewe. Kama msanii ametoa wimbo mpya, mashabiki hawataangalia iTunes ama ukurasa wake wa Twitter kupata link ya kununua wimbo huo ; wataangalia kwenye blogu kwajili ya kupakua bure.

Wasanii kimsingi wameruhusu wenyewe kuwa mtu wa kati katika mzunguko wa kutolewa kwa muziki wao.

Kutoa muziki wako bure ni mipango ya kiujanja. Nini kinatokea wakati wewe unaanguka kimuziki kutoka na maradhi au hauwezi tena kufanya matamasha ? fursa gani nyingine unaweza kuitumia kupata fedha ?

Katika miaka 20 ijayo wakati husikiki tena , wakati makampuni na biashara mbalimbali haziji kugonga mlangoni kwako, utawezaje kulipa bili zako ? Hakika haina maana kutarajia chanzo cha mapato yako kuwa matamasha pekee ?! Je, kweli unataka kuwa na umri wa miaka 60 na unafanya matamasha mala mbili kwa wiki, ukiimba juu ya vinywaji pengine muda huo havipo tena sokoni ?

Dunia inabadilika

Dunia inabadilika. “Streaming” inachukua utawala wa juu, na karibuni itakua njia kuu ya kupata muziki. Ukweli ni jambo zuri, ni jambo zuri kwa wasanii na sekta ya muziki. Kama matokeo ya fedha ya mwaka 2016 yalivyo onyesha, Streaming ni nzuri kwa ajili ya biashara ya muziki na mbaya kwa uharamia. Wateja wameonyesha kununua ni muhimu zaidi kuliko kutegemea bidhaa ya bure. Mashabiki wameacha kushusha nyimbo zisizo na ubora, matoleo ya wimbo ambayo yana jina la blog kwa sababu wametaka – ingawa bado ni uchaguzi pekee kwa baadhi ya watu. Lakini Streaming inaweza tu kuanguka kama thamani yake na gharama za usajili haziendani na matumizi.

Idadi kubwa ya watu katika bara la Afrika bado wapo miaka kadhaa nyuma, kwa sababu ya matatizo ya kitaasisi kama kusambaa kwa mtandao, gharama za kujiunga na mipangolio ya data, na kukosekana kwa chaguzi zenye faida kwenye huduma za Streaming. Zaidi ya hayo, wasanii wa Afrika bado wanategemea blogu kusambaza muziki wao, na kupuuzia kabisa chaguzi rasmi za usambazaji.

Kama mtu umejaribu kuratibu orodha ya kucheza muziki wa Afrika kwenye Apple Music, najua atakua wa kwanza kuniunga mkono kwamba idadi kubwa ya wasanii hawana muziki wao kwenye jukwaa hili au majukwaa mengine ya kulipia. Hii inafanya kuwa vigumu kwa mashabiki kununua muziki wao.

Narudia tena – urahisi wa biashara yako ni kila kitu. Kama mashabiki hawezi kununua albamu kwa urahisi kwenye majukwaa wanayotumia basi wataacha kuangalia kazi zako kabisa au kupakua kinyume cha sheria.

Dunia inabadilika na wasanii wa Afrika wanatakiwa kubadilika pamoja nayo. Mikakati yao haitakiwi kulenga ushindi wa muda mfupi ambao hauna thamani zaidi ya kelele wakati wanapuuzia mikakati ya muda mrefu ambayo sio tu itawawezesha kupata wasifu mzuri , bali itakua msaada kwenye maisha yao ya baadae.

Kama utamaduni utabadilika na uharamia ukashughulikiwa ipasavyo, basi wasanii wanatakiwa kuanza kupambana juu ya hatima ya maisha yao ya baadae sasa. Wanatakiwa kuwazoeza mashabiki kulipia muziki, au kuhamasisha mashabiki kuingia kwenye majukwaa ya Streaming na kupata muziki wao huko. Wasanii wanapaswa kushirikiana pamoja ili kupata ufumbuzi yenye faida ambao unaweza kufanya kazi katika nchi yao au eneo. Wanaweza kuifata mitandao ya simu na kuchunguza jinsi gani wanaweza kusambaza muziki wao huko kwa viwango nzuri. Wanaweza kuunda sheria za usambazaji wa bidhaa zao, sheria ambayo blogu lazima zizingatie. Kama blog inapata mapato ya matangazo kutokana na maudhui yako, labda blog hiyo inatakiwa kulipa msanii kwa haki hizo na si vinginevyo. Wasanii wanapaswa kuanza kuangalia faida ya kuwa na nguvu ya kuongozo mambo yao wenyewe.

SOMA NA HII:  Je Thamani Ya Mchezaji Inaweza Kuongezeka Kupitia Mitandao Ya Kijamii?

Dhibiti Maudhui yako

“Je unabadilika ama unakufa ?” Wasanii wanatakiwa kubadilika jinsi wanavyoingia kwenye soko la muziki na namna ya kuusambaza. Mbali na hilo licha ya kujiunga na majukwaa kama iTunes, Spotify na Bandcamp, wanapaswa pia kuzingati kutengeneza za kwao wenyewe.

Gharama za kuanzisha tovuti zimepungua kwa kiwango kikubwa. Leo msanii anaweza kujiunga na WordPress au Squarespace na kuwa na tovuti inayofanya kazi kikamilifu kwa gharama ndogo chini ya Shilingi laki moja kwa mwaka. Na kwa kiasi sahihi cha kujitolea, wasanii wanaweza kujifunza kwa urahisi jinsi ya kubuni tovuti zao wenyewe na kujisajili mtandaoni kwa muda wa chini ya wiki mbili. Tovuti inaweza kutumika kupandisha taarifa muhimu kuhusu msanii, ikiwa ni pamoja muziki wake mpya.

Kama msanii anataka kutoa nyimbo mpya bure, wanatakiwa kufanya hivyo kupitia majukwaa yao wenyewe; si kupitia blog, na dhahiri si kupitia datafilehost.

Mimi ni muumini wa imara kwamba kama wasanii wakubwa 20 (ambao wahahitaji blogu kuishi) wameamua kupiga chini kusambaza muziki wao bure na kuanza kusambaza muziki wao kwenye majukwaa yao wenyewe, blogu za kupakua muziki zitapoteza umuhimu wake.

Wasanii wanatakiwa kuangalia na kukusanya habari nyingi kadri iwezekanavyo kuhusu mashabiki wao. Wana kutembelea kutoka wapi, ni zipi anwani zao za barua pepe? Namba zao za simu ? Pia ni muhimu kuuliza: ‘Ninawezaje kuwalipa mashabiki kwa kuwa pamoja nami muda wote’.

Muombe shabiki anwani yake ya barua pepe kwa kubadilishana na bidhaa ya bure au maudhui ya kipekee ni njia bora ya kufanya biashara.

To be a successful creator you don’t need millions. You don’t need millions of dollars or millions of customers, millions of clients or millions of fans. To make a living as a craftsperson, photographer, musician, designer, author, animator, app maker, entrepreneur, or inventor you need only thousands of true fans. – Kevin Kelly

Kama msanii haitakiwi upewe bure taarifa kuhusu fanbase yako kutoka kwenye blogu ama huduma za kupakua muziki. Kama blog ipo tayari kujenga ushirikiano nawe na kukuhakikishia kiwango flani cha kukutangaza na kufika maeneo ambayo huwezi kufika peke yako, hilo ni jambo zuri na unapaswa kulifanyia kazi. Hata hivyo, inatakiwa uendelee kuomba taarifa za mwenendo wa muziki wako na uzielewe.

Blogu kwa upande mwingine – hapa wanahusika – wanatakiwa kuelewa jambo hilo kwa sababu utamaduni inabidi ubadilishwe. Jukumu letu kama ‘walinzi’ wa muziki ni kubadilika kuendana na wakati wa kuelekea kwenye huduma za ugunduzi wa muziki na vyombo vya habari vya kijamii . Mashabiki si kweli kwamba wanapenda tuwaambie msanii wanayempenda ametoa wimbo mpya wakati Google Now itawatumia taarifa moja kwa moja kwenye simu zao. Hawatahitaji sisi tuwaambia kuhusu Mistari bora ya Fid Q wakati Apple music wataweka orodha ya kucheza muziki ikiwa na maudhui sawa na hayo.

Kwa Marekani, asilimia 4% tu ya watu wote inagundua muziki mpya kupitia blogu. Ukilinganisha na asilimia 47% ambayo inagundua kupitia redio, hii ina maanisha wasanii wanatakiwa kuwekeza muda wao kuingia kwenye mzunguko wa redio kuliko kutoa kazi zao kwenye blogu.
Dunia inabadilika na sheria inaenda kwenye mwelekeo mpya. Kwa wale wanaojihusisha na utamaduni wa wizi wa kazi za wasanii wanaelekea sehemu mbaya.

Thamani halisi ya blogs kwenda mbele na kuwa bora ni kuweka mizizi katika uandishi wa habari.

Miaka 20 kutoka sasa wakati dunia inaangalia nyuma kwenye historia ya utamaduni wa muziki, itakutana na wingi wa makala zikielezea kuendelea kwa utamaduni, habari na ufafanuzi wa kitaalam, au watakutana na rundo la viungo maiti (dead links) za kupakua muziki na taarifa kwa vyombo vya habari za kunakiliwa?

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.