Sambaza:

Kurekodi simu unazopiga ama kupigiwa kwenye iPhone inaweza kuwa mtihani. Unatakiwa kulipa programu/app ambayo inawezekana tu kufanya kazi kwa kutumia dialer ya kawaida (au programu ya simu, ambayo haikusaidia ikiwa unahitaji kupiga simu kupitia WhatsApp, Skype, au huduma tofauti), au unaishia kutumia Rekodi ya tepi au simu nyingine kurekodi simu zako kupitia spika. Lakini PhotoFast inajaribu kurekebisha tatizo hili kwa kuleta adapta ya kurekodi simu.

Kifaa hiki unakiunganisha kwenye “port” ya iPhone yako na inaweza kurekodi simu zako kwenye kifaa chako kupitia huduma kama Skype, Facebook Messenger, Whatsapp, Line, Viber, na WeChat. Kifaa kinatumia format ya .m4a kwajili ya kurekodi, na unaweza kuchagua kuhifadhi faili kwenye hifadhi yako ya ndani au kadi ya microSD.

Kwa simu zinazoingia, kuna kitufe cha kurekodi moja kwa moja kwenye Call Recorder ambapo itaanza kurekodi moja kwa moja utakapo bonyeza. Pia inakuja na “3.5mm headphone jack”, hivyo inaweza kuwa kama adapta.


Sambaza:
SOMA NA HII:  Akaunti ya Twitter ya mwanzilishi wa McAfee VirusScan yadukuliwa

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako