KompyutaMicrosoft

Unaweza Kulipia Tsh300000 Kununua Keyboard hii?

Kama ningekuwa napata fedha nyingi zaidi ya ninazopata sasa , pengine, ningefikiria kununua keyboard hii. Ila kwa hari ya sasa:

Hata hivyo, Microsoft wameishinda Apple kutengeneza “wireless keyboard” yenye  “fingerprint scanner”. Fingerprint Scanner hii inakuwezesha kuingia (login) kwenye Kompyuta zinazotumia Windows 10 sambamba na tovuti kwa urahisi zaidi. Keyboard hii pia inafanya kazi katika “wired ama wireless mode”, tofauti na “Surface keyboard” ambayo ni wireless (Bluetooth) tu.

Inaendeshwa na “AAA batteries” mbili- seli za kuchaji pia zimewekwa – na zinadumu hadi miezi miwili baada ya kuzichaji. Keyboard hii ya kisasa inafanya kazi kwenye Windows 8, Windows RT, OS X 10.11.1, iOS 8, Android 4.2 na kuendelea. Hata hivyo, kufaida fingerprint Scanner yake, unatakiwa kuwa na  mashine inayotumia Windows 10, ambayo inawezesha Windows Hello. Yote haya itakugharimu $ 129 !

Microsoft pia wamezindua Microsoft Modern Mouse Mpya ambayo ina mwonekano kama wa Surface Mouse.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kuongeza Nafasi Kwenye Kompyuta
Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako