Kenya yatengeneza satelaiti yake kurushwa anga za juu Machi mwaka huu


Kenya imetengeneza setilaiti yake ya kwanza kabisa ambayo imepangiwa kurushwa anga za juu Machi mwaka huu.

Kenya

Wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi, wakisaidiwa na maafisa kutoka shirika la anga za juu la Japan walitengeneza chombo hicho katika mradi uliogharimu zaidi ya dola milioni moja.

Setelaiti hiyo itatumika kuchunguza mienendo ya kilimo, pamoja na kuchunguza maeneo ya pwani ya taifa hilo.

Japan ilitoa ufadhili na jukwaa la kuitengenezea lakini ni Wakenya wenyewe waliitengeneza.

Setlaiti hiyo itatumwa hadi Kituo cha Kimataifa cha Anga za Juu (ISS) mnamo mwezi Machi na kuzinduliwa rasmi kuizungukza dunia na roboti mwezi mmoja baadaye.

Hatua hiyo itaifanya Kenya kuwa miongoni mwa mataifa mengine saba barani Afrika yaliyo na setilaiti zinazoizunguka dunia.

Mataifa mengine ni Misri, Afrika Kusini, Morocco, Algeria, Nigeria, Mauritius na Ghana.

Kundi la wahandisi kutoka chuo kikuu cha Nairobi walioitengeza walikuwa kundi la kwanza kufaidika kutokana na mradi wa pamoja kati ya Umoja wa Mataifa na shirila la anga za juu la Japan unaolenga kuzisaidia taasisi za elimu kutoka mataifa yanayostawi kutengeneza setilaiti zao.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA