Kazi 7 Ambazo Zimechukuliwa na Teknolojia. Miaka 10 Ijayo Binadamu Ataishije?


Kadri miaka inavyozidi kwenda mbele, neno teknolojia linazidi kutawala ulimwengu hii imeonekana wazi kabisa. Kuna sekta chache sana katika ulimwengu wa sasa ambazo bado hazijatawaliwa na teknolojia.

Teknolojia inakuwa kwa kasi ya ajabu na kwa kila mageuzi, wanadamu wanakuwa kwenye nafasi ya kupoteza Ajira ambazo miaka ya nyuma zilikuwa ni kwajili ya utaalamu wao. Nakumbuka nimewahi kuangalia filamu za “science-fiction” ambapo robots wanapigana na wanadamu kugombania utawala wa taifa.

kazi

Jambo hili halipombali na kinachotokea, itatokea na itaendelea kutokea. Huku makampuni yakitafuta njia za kupata faida kubwa, wazo la kuwa na uwezo wa kutumia teknolojia kuchukua nafasi ya mwanadamu kwa kutumia kompyuta na robot ambayo inaweza kufanya kazi muda mrefu kwa gharama ndogo, kwa kasi zaidi na kusababisha makosa machache ni wazo zuri.

Robots pia inaweza kuwasaidia wafanyakazi ambapo zinaweza kufanya kazi kwa urahisi, zinazopendeza, au za hatari na kuacha kazi ambazo sio za automatiska kabisa, zinahitaji ubunifu, mawasiliano, na multi tasking kwa wanadamu.

Kwa miaka michache iliyopita, robots na kompyuta zimefanya maajabu makubwa katika utendaji na uwezo wao na kwa kiasi kikubwa zimepunguza kazi za binadamu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni na Chuo Kikuu cha Oxford , “Automation” inaweza kuchukua 47% ya kazi za sasa ifikapo mwaka wa 2033. Kwa hivyo, ikiwa unapanga kufanya kazi ambayo huenda ikadumu zaidi ya miaka kumi ijayo, basi kazi zifuatazo zitoe kwenye orodha yako. Kwa nini? Sababu ni kwamba kazi hizi zitakuwa automatiska (automated) na haja ya watu halisi kuchukua majukumu haya haitakuwepo kwa sababu teknolojia itaendelea kuchukua majukumu haya.

SOMA NA HII:  Baada ya kashfa thamani ya facebook yashuka kwa $58bn

Ifuatayo ni mifano ya kazi ambazo zinaweza kuchukuliwa na vifaa vya kiteknolojia:

1. BANK TELLER OPERATORS:

Ujio wa Mashine ya Automatic Teller ambazo sasa zinaweza kushughulikia amana za fedha (cash deposits) na kufanya kazi kama “tellers” kwa transactions hizo. Kuenea na / au maendeleo ya teknolojia hiyo ni lazima ifanya watu wenye jukumu hilo wakose kazi.

2. KARANI WA FEDHA (CASHIERS):

Hii inaonekana kama mfano dhahiri wa kazi ambayo inaweza kubadilishwa na mashine. Maduka mengi makubwa  yanatumia mashine binafsi ya checkout kinyume na makarani wa fedha wa kawaida na kwa kiasi kikubwa, matokeo yamekuwa chanya kwao. Kusambaa kwa “self-checkout machines” duniani kote, kutasababisha kazi kama karani wa fedha ibaki kuwa kwenye tishio kubwa kwa wanadamu.

3. MUHUDUMU WA MAPOKEZI (RECEPTIONIST):

Makampuni sasa yanaweza kuokoa fedha kwa kutokuajiri mtu kujibu simu shukrani kwa programu ya Virtual Receptionist. Nchi zingine zilizoendelea kiteknolojia zimepiga hatua zaidi kwa kujaribu robots halisi kutumika kama wapokeaji.

Kupiga simu yako na kupokelewa na mashine inaweza isivutie wengi, na hii ni moja ya sababu watu wa mapokezi kwa kiwango kikubwa hawajabadilishwa na kuwekwa mashine – bado.

Hata hivyo, hii haiwezi kupingana na ukweli kwamba hii ni moja ya kazi ambazo haziwezi kuendelea mbele zaidi au itafutika kabisa. Kama programu au robots zinaweza kutosheleza mahitaji ya kampuni husika, kujali jinsi wateja wao wanavyojisikia kuzungumza na mashine haitakuwa tatizo kubwa kwao hasa wakizingatia kuwa wanaweza kupunguza gharama.

SOMA NA HII:  Nissan imekuletea gari mpya kali zaidi inayotumia umeme!!

4. PACKING, STOCKROOM, NA WAREHOUSE MOVING:

Kazi zinazohusisha kuinua, kufunga au kusogeza bidhaa sasa zinachukuliwa na robots huku zikidhibitiwa na kompyuta. Makampuni kama Amazon, kwa mfano, hutumia robots zinazosafirisha bidhaa zote zinazotumwa kwa wateja.

Robots hizi huisaidia Amazon na wafanyakazi wake kufunga mizigo na kuisambaza kwa haraka zaidi kuliko wapinzani wake. Hata hivyo, wakati huo huo, robots hizi zimechukua kazi za wafanyakazi ambao wangeweza kushughulikia kazi hii.

Makampuni mengine pia hutumia mashine za forklift ambazo zinaweza pia kutumiwa kuhamisha, kupakia, na kupakua bidhaa.

5. RUBANI NA MADEREVA:

Ikiwa hujasikia kuhusu teknolojia ya gari zisizo na dereva au ndenge zisizo na rubani, huenda wewe ni “muhenga” na inapaswa usamehewa   1212ewew. “Autonomous drones” zinazofanya uchunguzi na hata kushambulia bila ya msaada wa wanadamu sasa hutumiwa na majeshi mbalimbali duniani kote.

Kwa kuwa teknolojia ya drones inazidi kukua zaidi, zinaweza kutumiwa kwenye maeneo mengine kama vile kutumika badala ya rubani kwenye ndege za mizigo. Tayari makampuni mengi ya usafirishaji yanatafuta njia ya kuacha kutumia marubani na kuanza kutumia mfumo wa kompyuta ambao utahitaji msaada mdogo wa binadamu endapo utahitajika.

SOMA NA HII:  Reji Robo hatua kubwa ya teknolojia iliyofikiwa na Japan

Kwa upande wa madereva, kuendelea kwa uboreshaji wa magari ya tesla, magari yanayojiendesha kuna uwezekano wa kuja kukubalika zaidi kuliko ilivyo sasa. Kwa hakika hii inaweza kuchukua muda, kama watu bado wanajiuliza kuweka maisha yao kwenye uaminifu wa robot, ambapo wengi wanasema zinaweza kuathiriwa na walaghai (hackers) . Bado kuna kazi ambazo haziwezi kujiepusha kuchukuliwa na teknolojia.

6. MFANYAKAZI WA BAA (BARTENDER):

Makampuni mengine tayari yana muundo huu kwenye ofisi zao. Roboti inaweza kutumikia kupeleka vinywaji vya pombe au kahawa kwenye meza za wateja. Kwa wale ambao wana hamu ya kutosha kuona jinsi hii inavyofanya kazi, nimewasogeza video ili kuona jinsi inavyowezekana kuletewa kinywaji na roboti.

Bonyeza hapa kuangalia Video.

7. TRAVEL AGENTS:

Kabla ya kuibuka kwa mtandao wa intaneti, kulikuwa na watu wengi ambao walifanya kazi kama wakala wa usafiri (travel agent) ili kusaidia kupata, kupanga na kutengeneza mpango bora wa kusafiri. Leo,kwa kutumia intaneti na kompyuta unaweza kufanya yote haya mwenyewe bila kuhitaji msaada wa “travel agent”.

Kuna kazi nyingine nyingi lakini kwa muda huu, nimeona ni bora orodha iwe fupi tu ili kuleta maana zaidi.

Je unaamini teknolojia inavyozidi kukua itasababisha watu wengi kukosa kazi ? Je kuna umuhimu wa mfumo wetu wa elimu kuboreshwa ili kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ? Tuandikie maoni yako kupitia sehemu yetu ya maoni hapa chini.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA