Home Nyingine Kauli Za Watu Maarufu Kwenye Maadhimisho ya Mwaka Mmoja Wa Mkuu Wa Mkoa Wa Dar, Paul Makonda

Kauli Za Watu Maarufu Kwenye Maadhimisho ya Mwaka Mmoja Wa Mkuu Wa Mkoa Wa Dar, Paul Makonda

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametimiza mwaka mmoja tangu achaguliwe na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli.

Mkuu wa mkoa huyo, amekutana na wadau mbalimbali wa mkoa huo kwa ajili ya kutathmini mambo mbalimbali. Viongozi mbalimbali wa Serikali na watu wengine maarufu wakiwemo wakali kutoka kwenye industry ya Bongofleva walipewa nafasi ya kuzungumza. Hizi ni baadhi ya kauli zao:

Kamanda Sirro amezungumza kuhusu ishu ya Dawa za Kulevya.

 

Awali ya yote Kwanza nimpongeze Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda kwa kutimiza mwaka mmoja lakini pia nimpongeze kwa kuwaleta vijana wetu hasa wale waliokuwa wanatumia madawa ya kulevya. Kwangu ni siku ya furaha kwasababu tangu hili zoezi lianze hata nikiwapigia simu wasanii kama wakina Banana Zoro hawapokei simu, hata viongozi wa dini hivyo hivyo lakini hii inaonesha kwamba kila mtu anajua umuhimu wa suala hili.

Langu ni moja tu, kazi hii ni kubwa. Watu waendelee kutoa taarifa. Nina jambo moja tu kwa viongozi. Mkoa wa Pwani viongozi wengi wanauawa. Tuna changamoto Tanga na hata Mwanza>>>Simon Sirro

Msanii kutoka Bongoflevani Diamond Platnumz naye alipata nafasi ya kuzungumza:

Kwanza nimpongeze kaka yangu TID, kwa sababu unapokuwa mwanamuziki ukasimama mbele za watu ukasema mimi nilikuwa nafanya lakini sasa hivi nimekuja katika njia nzuri ni kitu cha kumpongeza sana. Na mimi naamini kabisa ngoma yangu itakayotoka na TID itakuwa ngoma kubwa sana,”

Najua watatupinga sana lakini ukiona mtoto analia sana ujue kuwa viboko vimemuingia na ukiona watu wanapiga kelele sana ujue kuwa kampeni yetu imefanikiwa na kufanikiwa ndio dhumuni letu sisi>>> Diamond Platnumz

TID naye alipata nafasi ya kuzungumza:

Ningependa niwe mfano wa mambo mema yanayofanyika mkoa wa DSM na Tanzania nzima.

Baadhi ya wasanii wanaona njia niliyoichagua siyo sawa, sidhani kama ni wakati wa kukataa ukweli haiitaji hata kwenda chama kingine.

Sidhani kama kuna chama kinaweza kukubali msanii mwanamuziki anayetumia dawa za kulevya awepo kwenye chama chao

Haihitaji uwe mwanasiasa ili kukemea matumizi ya dawa za kulevya, hii inahitaji uwe mtanzania kwanza kwa sababu ili ni janga ni la taifa>>>TID

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar naye amesema:

Sasa RC Makonda umekomaa, haiwezekani kila anayekuchokoza ukamjibu.

Tuwatazame mateja kama ndugu zetu, tusiwaue wala kuwachoma moto wafanyapo uhalifu bali tuwape msaada wanaoutaka.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *