Nyingine

Kauli ya Nay wa Mitego na Zitto baada ya Roma kukamatwa

Baada ya Mkali wa Bongo Fleva Joseph Haule ‘Proffesa Jay’ kutoa taarifa ya kukamatwa kwa rapper Roma Mkatoliki na Moni Central Zone katika studio za Tongwe Records na watu wasiojulikana. Watu mbalimbali wakiwemo mastaa na wanasiasa wameumizwa na kitendo hicho na kutoa yao ya moyoni.

Kupitia account yake ya Instagram rapper Nay wa Mitego ameyaandika haya.

”Kuvamia Ofisi Za watu, heh.! Kumbe nayo ni Kazi.?! Nina Imani uko salama mwanangu, Kamanda @roma2030 Sina ata chembe ya wasi wasi. #Wapo.” – Nay wa Mitego.

 

Naye Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika:

”Uvamizi wa studio ya Tongwe na kumkamata msanii Roma Mkatoliki ni mwendelezo wa uongozi wa kigangstar na lazima kulaani Kwa nguvu zetu zote.” – Zitto Kabwe.

SOMA NA HII:  Kwa nini Mwanamke Anaweza Kuweka Picha Zake Za Uchi Kwenye Simu Yake? - Uzoefu Binafsi

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.