Katika Mbio za Kurejea Uaminifu Wako: Hapa kuna Mabadiliko 6 yatakayofanywa na Facebook, lakini Je, Yatosha?


Hivi karibuni, Mark Zuckerberg alivunja ukimya wake wa siku tano kuhusu kashfa ya Cambridge Analytica ambayo ilionyesha jinsi sera za kugawana data kwenye Facebook zilivyosababisha Analytica kuingilia data binafsi za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.

Katika chapisho la Facebook, Mark Zuckerberg ameeleza hatua zitakazochukuliwa ili kuhakikisha usalama wa data zako kwenye jukwaa hilo, ni pamoja na:

  • Kuchunguza mitandao yote ambayo inashirikiana na Facebook kabla ya kufanyiwa mabadiliko ya mwaka 2014 ya namna ya kuweza kupata taarifa ya watumiaji.
  • Utakuwa na uwezo wa kuona programu zinazoweza kufikia data zako na zitaondolewa moja kwa moja ikiwa hujatumia app ndani ya miezi 3.
  • Kizuizi cha upatikanaji kwa apps zinazohitaji Facebook login. Kuleta maboresho, kampuni itazuia data inayoshirikishwa kuwa jina, barua pepe na picha ya wasifu tu. Ikiwa msanidi programu anahitaji upatikanaji zaidi wa data, haipaswi tu kupata idhini bali pia kuingia mkataba.
  • Kama ilivyoelezwa katika pointi ya 2, Facebook itaanzisha kipengele kipya juu ya news feed yako ambacho kitakuwa kinaonyesha apps zote zilizo na data zako ili iwe rahisi kuondoa ruhusa zao.
  • Mpango wa kupanua bug bounty program yake ili kuvutia watafiti zaidi wa usalama na kuboresha usalama wa jukwaa.
  • Mwisho, taarifa itatumwa kwa watumiaji wote ambao data zao zimetumiwa vibaya wakati wa kashfa ya Cambridge Analytica.

Sasa, watu wengi mtandaoni wanasema kwamba Mark Zuckerberg hajajibu swali kuu, yaani, kwa nini Facebook ilikuwa kimya juu ya kashfa hii ilivyoanza kuibuka mwaka 2015.


Toa maoni yako, je hatua hizi zinatosha kabisa kwa wewe kuamini Facebook tena?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA