Sambaza:

Wanafunzi na wazungumzaji wa Kiswahili na Kiingereza wamekuwa wakipata matatizo kutokana na kukosekana kwa kifaa cha kurejelea kinachoakisi hali ya sasa ya lugha ya Kiswahili. Hapa nakuwekea kamusi ya TUKI ambayo imekusudiwa kuziba pengo hilo.

Kamusi hii imetayarishwa na wataalamu wa leksikografia wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Aidha, imepitiwa na kuhakikiwa na wataalamu wa lugha na isimu kutoka vyuo vikuu mbalimbali vya Tanzania na Kenya.Uandishi wa Kamusi hii ulianza rasmi mwaka 1997 na kukamilika mwaka 2000. Ina vitomeo (maneno yanayofafanuliwa) zaidi ya 30,000.

SOMA NA HII:  Kenya yatengeneza satelaiti yake kurushwa anga za juu Machi mwaka huu

Kamusi hii itawafaa wanafunzi wa sekondari na vyuo, wakufunzi wa lugha, walimu, wataalamu na wazungumzaji wote wa lugha za Kiswahili na Kiingereza.

Bonyeza link hapa chini kupakua Kamusi ya TUKI: Kiingereza – Kiswahili/ Kiswahili – Kiingereza

Kamusi ya TUKI: Kiingereza – Kiswahili/ Kiswahili – Kiingereza

Ahsante.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako