Sambaza:

Hivi karibuni mamlaka ya mawasiliano hapa Tanzania TCRA ilitangaza kuzitoza faini kampuni sita 6 za simu kutokana na utoaji mbovu wa huduma za simu, kampuni ambazo zilizotozwa faini hiyo ni pamoja na kampuni za Airtel ambayo imetozwa faini ya Sh1.08 bilioni), Smart (Sh1.3 bilioni), Vodacom (Sh945 milioni), Zantel (Sh105 milioni) pamoja na kampuni ya Halotel (Sh1.6 bilioni).

kampuni

Aidha mamlaka hiyo ilizitaka kampuni hizo hadi kufikia tarehe 14 Oktoba mwaka huu kampuni zote ziwe zimesha lipa faini hiyo.

Hivi karibuni ripoti kutoka kwenye gazeti la mwananchi zinasema Kampuni sita za simu zilizotozwa faini na Mamlaka hiyo zimetii sheria bila shuruti ndani ya muda uliopangwa. Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, James Kilaba alisema licha ya kulipa faini, kampuni hizo zimefanya maboresho ya mtandao katika maeneo yaliyokuwa yanasumbua.

SOMA NA HII:  Zitto Kabwe: Sakata la Airtel ni kama NBC

Mwezi Julai, TCRA ilizitoza faini kampuni hizo baada ya kushindwa kuzingatia taratibu za usajili wa laini za simu za mkononi baada ya kubainika wateja wengi kutumia vitambulisho visivyotambulika na kusababisha kukiuka taratibu za usajili wa laini za simu kwa ujumla.

Kampuni zote zimefanikiwa kulipa faini hiyo ikiwa pamoja na ile ya makosa ya kurudia ambapo kampuni ya Tigo nayo ilihusika kwa kulipa kiasi cha Sh625 milioni huku kampuni nyingine za kama Halotel ambayo ilitozwa Sh822 milioni, Airtel Sh542 milioni, Zantel Sh52 milioni na Smart Sh37 milioni kwa sababu ya makosa hayo hayo ya kujirudia.

SOMA NA HII:  NOTICE OF INTENTION TO INITIATE A SPECTRUM ASSIGNMENT PROCESS FOR 700 MHz BAND

Hivi sasa mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imekuwa na sheria kali huku ikiwataka wananchi kuwa makini na matumizi ya mitandao kwa kuanzisha kampeni mbalimbali ikiwa pamoja na ile iliyozinduliwa mwezi uliopita ya kudhibiti maudhui yasiyofaa kwenye mitandao ya kijamii.

Chanzo : Mwananchi

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako