Huu ni ushirikiano mkubwa wa kwanza chini ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Uber Dara Khosrowshahi.

Katika ushirikiano wa kwanza wa bidhaa chini ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Uber Dara Khosrowshahi, kampuni hiyo leo imetangaza rasmi kuingia kwenye biashara ya credit card. Uber imeungana na Barclays na VISA kutoa kadi ya Uber credit card.

Kwa kawaida, credit card hiyo ya Uber itakuwezesha kulipia huduma za usafiri za Uber, na utarudishiwa asilimia 2% ya fedha ulizolipa (mpango huo pia utafanya kazi katika ununuzi wa bidhaa mtandaoni ikiwa ni pamoja na video na huduma za kusambaza muziki).

SOMA NA HII:  Taarifa kutoka TANESCO kuhusu mfumo wa ununuzi wa umeme kwa njia ya LUKU

Lakini itakupa 4% ya fedha ulizotumia kulipia vyakula migahawani, takeout, na baa, ikiwa ni pamoja na UberEats na utarudishiwa fedha 1% kwenye manunuzi ya kawaida. Pia inatoa fedha ulizotumia 3% kwenye huduma za ndege na hoteli.

Watumiaji wataweza kufanya maombi ya kupata kadi hiyo kwenye Uber app kuanzia mwezi Novemba.

Kadi ya Uber haina ada ya kila mwaka na hutoa ziada ya $ 100 baada ya kutumia dola 500 ndani ya siku 90 za kwanza.

Uber si kampuni pekee ya teknolojia inayotoa credit card. Apple pia inatoa kadi kama hiyo na ina viwango sawa vya riba, pia imesaidiwa na Barclays.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako