Kampuni ya Toyota Kutoka Japan Kutengeneza Gari za Mbao


Ikiwa nchi mbalimbali duniani zimeanza kufanya utafiti wa kutengeneza magari yasiyotumia mafuta, Japan pia imeanza kufanya utafiti wa kutengeneza magari ya mbao ngumu.

Toyota kutambulisha gari lilotengenezwa kwa mbao na teknolojia ya kiutamaduni ya nchini Japan isiyohusisha utumiaji wa misumari wala nati katika kuzishikilia mbao hizo.

Sersuna – Gari la mbao kutoka Toyota

Wataalamu wanaeleza kuwa lengo kubwa ni kupunguza uzito wa magari pamoja na athari za hewa chafu na kelele ambapo watafiti katika Chuo Kikuu cha Kyoto wameeleza kuwa mbao kwa karne nyingi imetumika kutengeneza meli, nyumba na mengineyo na hivyo gari hizo za mbao zitakua na ubora uleule kama magari ya metali lakini yatapungua uzito kwa asilimia 80.

Huko nchini Japan kuna mahekalu ya kitamaduni ambayo huvunjwa na kujengwa upya kila baada ya miaka 20. Kitu cha pekee katika ujengaji wa hekalu hizo no utumiaji wa mbao usiohusisha utumiaji wa ata msumari mmoja katika ujenzi wake.

Ubomoaji na ujengaji wa mahekalu hayo umekuwa ukifanyika kwa takribani miaka 1,300 sasa , na huwa wanabomoa na kujenga tena ili kuhakikisha majengo hayo yanaendelea kuwa na nguvu na usalama. Teknolojia ya ujengaji huo inapitia kwa vizazi hadi vizazi, na sasa Toyota wanatumia teknolojia hiyo katika utengenezaji wa gari.

Aina kadhaa za mbao zimetumika kutengeneza bodi la gari hilo, chasis, viti, uskani (steering wheel) na rim za matairi.

Hili linategemewa kuanza kufanyiwa utekelezaji kuanzia miaka 10 ijayo ikiwa ni pamoja na tafiti kuhusu kutengeneza magari ya material ya plastic ambayo yatakuwa rafiki kwa joto na kuchukua nafasi ya magari ya metali.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA