Mawasiliano

Kampuni ya Simu ya TTCL yafutiwa deni la Sh76 bilioni

on

Kampuni ya simu ya TTCL ambayo inaongoza kwa utoaji huduma wa simu za mezani hapa nchini, hivi karibuni imepewa msamaa wa deni ililokuwa inadaiwa na serikali ya Tanzania.

TTCL

Deni hilo ambalo lilikuwa linafikia shilingi za Tanzania bilioni 76 limesamehewa rasmi na waziri wa fedha na mipango wa hapa Tanzania Dr Philip Mpango. Hata hivyo waziri huyo alibainisha kuwa deni hilo sasa limebadilisha na kuwa mtaji ambapo sasa fedha hizo zitaenda kutumiaka na kampuni hiyo ya TTCL kama mtaji wa kukuza kampuni hiyo.

Aidha kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 5(3) na 9 cha Sheria ya Fedha ya Tanzania, Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango alibadilisha deni hilo kuwa mtaji kuanzia mwezi Agosti mwaka huu.

SOMA NA HII:  #MHKutokaMaktaba!! Tujikumbushe Watangazaji wa Zamani wa Redio na TV

Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano inasema lengo la kugeuza mkopo huo kuwa mtaji ni kuitaka TTCL kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, tija na weledi ili kuongeza ushindani katika soko.

Chanzo : Mwananchi

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.