Kampuni ya Samsung Yazindua Diski ya SSD Kubwa Zaidi Duniani


Kampuni ya Samsung yenye makao yake makuu nchini Korea ya Kusini hivi leo imevunja rekodi kwa mara nyingine tena kwa kuja na diski ya SSD kubwa kuliko zote duniani. Samsung ndio walikuwa wameshikilia rekodi ya utengenezaji wa diski ya SSD yenye ujazo mkubwa zaidi.

Rekodi hiyo waliiweka mwaka 2016 walipozindua hard disk yenye  uwezo wa TB 16 sawa na GB 16,000 (hard disk kubwa zaidi kwa kipindi hicho), lakini pia kampuni ya Seagate ilishakuja na Hard Disk ya TB 60 ambayo haiku fanikiwa kuwafikia wanunuzi na ilikuwa kama sehemu ya maonyesho pekee ukitofautisha na Hard Disk hii ya Samsung.

 

Diski yao mpya aina ya SSD au Solid-state drive ina uwezo au ukubwa wa Terabyte (TB) 30.72 ambayo ni sawa na GB 30,000. Pia ina ukubwa wa inchi 2.5 tu. Katika utendaji kazi toleo hili ni bora zaidi, uhamishaji wa mafaili (copying/transfer) ni karibia mara mbili zaidi ukilinganisha na toleo la TB 15.36 – kasi ya usomaji na uhamishaji mafaili wa MB 1,700 hadi MB 2,100 kwa sekunde.

Hard Disk hiyo imetengenezwa kwa vitufe maalum vinavyoitwa NAND ambavyo vipo zaidi ya 30 ambapo kila kitufe kimoja kina uwezo wa terabyte 1 TB ambavyo ni sawa na kusema hard disk hiyo inauwezo wa kuhifadhi filamu za HD za ukubwa wa GB 1 zaidi ya filamu 5,700 au zaidi.

Hard disk hiyo iliyopewa jina la PM1643, inasemekana kuja na warrant ya miaka mitano yani maana yake ni kuwa ikiharibika ndani ya miaka mitano unaweza kupewa nyingine au kufanyiwa marekebisho. Hii inaonyesha kuwa samsung inajiamini sana kwenye utengenezaji wa Hard Disk hiyo. Bei bado haijajulikana lakini inatarajiwa kuwa na bei kubwa….Samsung wanampango wa kutumia teknolojia hiyo kutoa tena matoleo ya ujazo mdogo kwa bei nafuu pia kuliko zamani.

2 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA