Kampuni ya Amazon sasa ina ukubwa sawa na nchi ndogo


Wafanyakazi wa Amazon sasa ni wengi zaidi kuliko idadi ya watu kwenye baadhi ya nchi ndogo.

Siku ya Alhamisi, kampuni hiyo ya e-commerce ilieleza kwamba imeajiri watu 541,900 mwishoni mwa robo ya tatu ya mwaka huu. Hiyo ni idadi kubwa zaidi kuliko wakazi wa nchi 63 ulimwenguni kote, ikiwa ni pamoja na nchi zinazojulikana kama Iceland na Bahamas. Kwa mfano, Belize, ina idadi ya watu 347,369 tu.

SOMA NA HII:  Vodacom Yasitisha Huduma za Kununua Umeme za Luku

Kama tunavyoona katika chati hii kutoka Statista,, ambayo inategemea data kutoka kwenye kampuni yenyewe, Amazon imekuwa ikikua kwa kiwango cha haraka. Iliongeza watu 159,500 ndani ya miezi mitatu kati ya mwishoni mwa Juni na mwisho wa Septemba. Wengi walikuja baada ya kampuni hiyo kununua biashara ya Chakula, lakini Amazon iliajiri makumi ya maelfu ya wafanyakazi wa ziada.

Kampuni ya Amazon

Na haijaishia hapo. Kampuni hiyo ambayo ni kubwa mtandao pia ilitangaza mipango ya kuajiri wafanyakazi wa muda 120,000 msimu huu wa sikukuu kufanya kazi kwenye maghala yake ya Marekani na vituo vya huduma za wateja na inatarajia kuwapa kazi za kudumu wafanyakazi hawa wa muda. Wakati huo huo, kampuni hiyo imesema wakati inafungua makao makuu yake ya pili, ina mpango wa kuongeza kazi nyingine kama 50,000 kwenye ofisi hizo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA