Mambo 5 Muhimu Kampuni Nyingine Zinapaswa Kujifunza Kutoka Kwa Tecno mobile


Kampuni ya kutengeneza simu za mkononi kutoka nchini China, Tecno Mobile imeibuka kutoka kuwa kampuni ndogo hadi kuwa moja ya bidhaa kubwa katika soko la simu za mkononi la Tanzania.

Tecno Mobile ilipoingia Tanzania, soko lilikuwa linatawaliwa hasa na Nokia na Samsung. Miaka ya nyuma, Nokia alikuwa Mfalme wa simu za mkononi. Ilikuwa ngumu kufikiria jinsi Tecno itakavyoweza kupambana dhidi ya Nokia na wazalishaji wengine wa simu za mkononi.

Licha ya utawala wake katika soko, simu za Nokia zilianguka kutokana na bei zake; simu zao zilikuwa za bei kubwa. Kulipia Tshs 100,000 kununua simu ambayo haina uwezo wa kufanya vitu vingi zaidi ya kucheza muziki ilionekana kama kitu cha ajabu hasa pale simujanja kama Huawei U8150 Ideos zilipoanza kuingia kwenye soko. Tecno walitambua hili na wakatoa simu kadhaa za kawaida ambazo zilikuwa karibu na nusu ya bei ya simu za Nokia. Lakini hawakuishia hapo. Baadaye walitangaza ujio wa simujanja zao za bei nafuu kama Tecno P3 na N3 ikiwa ni jitihada za kutawala soko la simu za bei nafuu na kuongeza upatikanaji wake katika soko la simujanja.

tecno mobile

Miaka michache baadae, Tecno Mobile sasa iko juu kwenye Soko la simu nchini Tanzania na bidhaa nyingine maarufu kama Samsung wanawaangalia kama mshindani mkuu. Tecno imeimarisha kwa uangalifu bidhaa zake na kutengeneza chaguo mbadala kwa kizazi cha sasa kinachotaka bidhaa zenye ubora kwa bei nafuu.

Yafuatayo ni baadhi ya mambo machache ambayo bidhaa nyingine zinaweza kujifunza kutoka kwa kampuni ya Tecno:


Fahamu Soko lako kuu/Fahamu wateja wako

Katika biashara, pendekezo lako la thamani linapaswa kuendana na soko unalolilenga ; unapaswa kutambua soko kuu la bidhaa zako na kuelewa mahitaji ya soko husika. Tecno inalenga sana wateja wa soko la Afrika, soko ambalo limekuwa likisahauliwa na makampuni mengi ya kutengeneza simujanja.

Tecno Telecom Limited ilipoanzishwa mwaka 2006, biashara yao ililenga soko la Asia ya Kusini . Baada ya kujifunza mahitaji ya masoko katika mabara ya Amerika ya Kusini, Asia ya Kusini Mashariki na Afrika, waligundua kwamba Afrika itakuwa soko lenye faida zaidi kwa shughuli zao. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, bidhaa nyingi zinazoletwa Afrika hazijatengenezwa kwajili ya mahitaji ya hapa, kwa hiyo lengo lao ni kuzalisha vifaa maalum kwaajiri ya soko la Afrika.


Tengeneza bidhaa imara kwa bei nafuu

Simu ya Tecno Camon C5

Bei ya chini italeta faida kwa muda mrefu kama ubora ni mzuri. Watengenezaji wengi wa simu za mkononi hutoa vifaa vya pande zote mbili kwa lengo la kujiimarisha katika kila soko. Unapotaka kutoa bidhaa mpya, inapaswa kuwa kitu ambacho ni cha kipekee na wewe (brand), unapaswa kujivunia. Wakati huo huo, bidhaa hiyo inapaswa kuwa ya bei nzuri.

Mwaka huu Tecno imetoa bidhaa kubwa za aina mabalimbali. Imetoa simujanja za bei nafuu  zenye ubora unaovutia watu wengi (skrini 720p, uunganisho wa 4G, processor bora na kamera ya kushangaza).

Bei ni kipengele muhimu sana na ni ajabu kwamba baadhi ya watengenezaji wa simu bado wanauza vifaa vyao kwa bei isiyo ya kawaida. Kwa mfano, siwezi kuelewa ni kwa nini kampuni kama Oppo, iliyoingia hivi karibuni katika soko la Tanzania imetoa simu ya kawaida kama Neo 3 na bado inaiuza kwa bei sawa na Camon C5.


Kuwa na mfumo sahihi wa usambazaji

Tecno haikuingia kwenye soko na fanfare kubwa kama biashara nyingi zinavyofanya. Kulikuwa na taarifa ndogo juu yao kwenye mtandao lakini bado simu zao zilikuwa zinauzwa na kufika mikononi mwa watu mitaani ya Bongo.

Kuingia kwenye soko la Tanzania, walishirikiana na wafanyabiashara kadhaa wa simu na wauzaji. Karibu kila duka la simu katika mitaa ya Uhindini Mbeya, Kariakoo Dar es Salaam, na kwingineko vifaa vyao vilipatikana na kwa njia hii waliweza kuuza bidhaa zao kwa wingi.

Nembo ya Tecno katika maeneo ya kariakoo

Tengenezea matangazo ya kisasa na yenye nguvu zaidi

Kampuni nyingi za simu zinauza bidhaa zao kwa bei ya juu ila kupata faida kubwa kuweza kufidia gharama za matengenezo. Gharama moja kubwa ni matangazo – Inagharimu kiasi kikubwa cha fedha kulipa aina za kawaida za matangazo kama vile matangazo ya gazeti, mabango, matangazo ya TV na kadhalika. Makampuni mara nyingi husahau tuna chombo chenye nguvu sana ambacho kina gharama nafuu – intaneti.

Tecno ilipoingia katika soko la Tanzania, hawakuwa wanajitangaza vizuri hasa mtandaoni. Vitu vimebadilika tangu wakati huo, brand yao sasa inafanya kazi zaidi mtandaoni; brand inafanya kazi kwenye Facebook, Twitter na pia ina msingi wa shabiki kwenye Instagram. Uwepo wao mkubwa kwenye mitandao ya kijamii umesaidia kampuni kujitangaza zaidi na kuonyesha bidhaa zao.


Kuingia kwenye makundi mengine ya bidhaa

Tecno Mobile haikuishia kwenye simu. Kampuni hiyo ilielewa umuhimu wa kupanua biashara kwa kutoa bidhaa zaidi ya simu na hivyo ilianza kutoa Android tablets za bei nafuu kwenye soko. Miaka ya karibuni Tecno imeingia kwenye biashara kubwa zaidi – kampuni imeingia kwenye biashara ya vifaa vya windows. Hivi karibuni, walishirikiana na Intel na Microsoft ili kuzindua WinPad 10, laptop/tablet yenye gharama nafuu kwajili ya watumiaji ambao wanatafuta kifaa kinachokidhi mahitaji yao ya kazi.

Tecno WinPad 10.

Watumiaji wa simu za mkononi hubadilisha mitazamo na mahitaji ya aina ya kifaa kipya wanachotaka kununua kutokana na gharama. Kwa sababu bidhaa zao ni imara na zinauzwa kwa bei nzuri, Watanzania wataendelea kuipenda Tecno Mobile. Nani anajua, mashabiki wao huenda siku moja watakuwa wanajivunia brand hii kama Apple fanboys.

Toa maoni yako juu ya Tecno Mobile na simu zake.  Tuambie mawazo yako katika sehemu ya maoni hapa chini!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA