Sambaza:

Kuna kampuni nyingi zinazotoa huduma bora za kuagiza magari ya nje hapa Tanzania, lakini kununua mahali fulani kunaweza kukupa uhuru zaidi wa kupumzisha akili yako juu ya ununuzi wako mpya. Magari si mashati au viatu kwamba ikiwa haifai, unaweza kurudisha tu au ubadilishane na yenye ubora zaidi  au kupata marejesho.

magari ya nje

Unapotaka kununua gari, unapaswa kukumbuka kwamba kuna hatua nyingi zinazohusika zaidi ya kutembea hadi sehemu ya mauzo ya magari, kuchagua gari, kubadilishana fedha kwa funguo na kufurahia kurudi nyumbani na usafiri wako mpya. Mchakato mzima haufanyi kazi kama hivyo.

SOMA NA HII:  Nissan imekuletea gari mpya kali zaidi inayotumia umeme!!

Kwa kusema hayo, hizi ni kampuni mbalimbali zinazoweza kukusaidia kuagiza magari ya nje hapa Tanzania.

Car Junction

Kampuni ya Car Junction inauza magari kutoka nchini Japani pia inauza magari ya kibiashara na vipuri vya magari jijini Dar-es-Salam, Tanzania. Car Junction inauza magari yaliyotumika  kwa bei nafuu sana. Inasafarisha magari yaliyotumika kama vile Toyota, Honda, Mazda, Mitsubishi, Nissan, Isuzu, Suzuki nk Sisi pia inauza trekta mpya na zilizotumika za Massey Ferguson na zana nyingine za kilimo nchini Tanzania.

Nunua magari ya Kijapani yaliyotumika (second-hand cars) kutoka Car Junction Tanzania. Ina orodha ndefu ya magari yaliyotumika, magari ya kibiashara na vipuri kwa bei nafuu.

Tovuti: www.carjunction.com

Be Forward

Ilianzishwa Machi 10, 2004 na Hironori Yamakawa. Inauza na kusafirisha magari yaliyotumika na auto-parts katiaka nchi zaidi ya 124 duniani kupitia tovuti yake ya biashara kwa njia ya intaneti (E-Commerce). Operesheni yao kuu, kusafirisha magri yaliyotumika, imesafirisha magari 12,000 kama kiasi cha mauzo ya kila mwezi na magari 146,925 kama kiasi cha mauzo ya kila mwaka kwa mwaka wa fedha wa hivi karibuni (mwezi wa Julai, 2015).

BE FORWARD inauza magari yaliyotumika yakiwa bado yapo kwenye ubora mzuri nchini Tanzania pia inatoa huduma ya “clearing and delivery” katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania kupitia ofisi zake jijini Tanzania.

Tovuti: www.beforward.jp

SBT Tanzania

SBT ni mojawapo ya kampuni za biashara ya magari zinazoongoza ina makao makuu yake huko Yokohama, Japan. Magari kwenye mtandao wao ni magari yaliyotumika katika nchi za Japan, Korea ya Kusini, Marekani, Ungereza, na Ujerumani ina machaguo bora zaidi. Ina taratibu nyepesi na za haraka za kumfikishia mteja gari lake. Sasa ina ofisi  katika nchi 15 kwa lengo la kutoa huduma bora zaidi duniani kote. SBT ni muuzaji wa magari kimataifa tangu 1993.

Tovuti: www.sbtjapan.com

SOMA NA HII:  Nissan yaja na teknolojia mpya ya kupunguza ajali za barabarani

Autocom Japan

Autocom Japan ni kampuni ya kuagiza magari ya Kijapani ambayo imewekeza katika kuuza magari yaliyotumika yenye ubora wa juu katika nchi nyingi duniani kote. Imeimarisha mtindo wake mpya wa biashara ambao ni kusimamia hatua zote muhimu katika kuleta gari lako kutoka Japani hadi nchini mwako, kwanzia ununuzi wa magari hadi kupanga usafirishaji wake.

Tovuti: autocj.co.jp

Tradecarview

Carview ilianzishwa mwaka wa 1996 kama mtoa huduma wa habari za magari mtandaoni. Carview inashirikisha habari tofauti za magari na makampuni na watumiaji kupitia mtandao na hivyo kuongeza ubora wa kuhudumia wateja. Lengo lao kuu ni kuleta mapinduzi ya usambazaji kwenye soko la magari la kimataifa.
Tangu kuanzishwa kwa, Carview Corporation (carview.co.jp) imekuwa ikitambulika kama moja ya tovuti kubwa za magari nchini Japan ambayo inawapa watumiaji habari kamili za kununua gari.

Tovuti: www.tradecarview.com

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako