Nyingine

kamishna jenerali wa uhamiaji afanya mabadiliko makubwa ya viongozi wa mikoa nchini

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dk Anna Makakala, amefanya mabadiliko makubwa ya viongozi wa Idara ya Uhamiaji wa mikoa mbalimbali pamoja na kuwateua viongozi wapya wa mikoa kushika nyadhifa hizo kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar.

Katika mabadiliko hayo amewapangua vigogo waliokuwa mikoani na kwenda mikoa mingine kama inavyoonekana kwenye mabano, ambapo Naibu Kamishna wa Uhamiaji Sixstus Nyaki (Mwanza) anakwenda Simiyu, Naibu Kamishna wa Uhamiaji Selemani Kameya (Rukwa) anakwenda Tabora.

Mkuu wa Uhamiaji Naibu Kamishna wa Uhamiaji, Asumsio Achacha (Mbeya), amehamishiwa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mkuu wa Uhamiaji Naibu Kamishna, Peter Kundy (Manyara) anakwenda Dodoma kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi Ali Mohamed ambaye amehamishiwa Arusha.

Taarifa hiyo ya Uhamiaji, ilieleza kwamba Naibu Kamishna wa Uhamiaji Mkemi Seif ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja huku Naibu Kamishna wa Uhamiaji Muhsin Abdallah Muhsin akiteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Naibu Kamishna wa Uhamiaji Said Hamdani ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mjini Magharibi.

“Naibu Kamishna wa Uhamiaji Othman Khamis Salum ameteuliwa kuwa Mkuu wa Uhamiaji Mjini Magharibi Unguja. Katika mabadiliko hayo baadhi ya Wakuu wa Uhamiaji wa mikoa wamebaki katika vituo vyao vya kazi vya awali akiwemo aliyekuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Morogoro Naibu Kamishna wa Safina Muhindi, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Lindi na Naibu Kamishna wa Uhamiaji George Kombe anakuwa Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Ruvuma.”

SOMA NA HII:  Unatumia "Lock ? " ya aina gani kwenye simu yako?

“Naibu Kamishna wa Uhamiaji Hilgaty Shauri, Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Singida, Naibu Kamishna Faith Ihano na Mkuu wa Uhamiaji Mkoa wa Mara Naibu Kamishna Fredrick Eustace Kiondo,” imeeleza taarifa hiyo.

Wengine waliobaki kwenye vituo vyao vya awali ni pamoja na Naibu Kamishna Abdallah Towo (Kagera) na Naibu Kamishna Anastazia Ngatunga (Shinyanga).

Katika mabadiliko hayo Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dk. Makakala pia amewateua viongozi wa uhamiaji wa mikoa ambao ni Naibu Kamishna Mary Palmer (Dar es Salaam), Naibu Kamishna Plasid Mazengo(Pwani), Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji James Mwanjotile(Mtwara), Kamishna Msaidizi Mwandamizi Hope Kawawa (Iringa), na Kamishna Msaidizi wa Uhamiaji Hosea Kagimbo (Njombe).

Wengine ni Naibu Kamishna Rashid Magetta (Songwe), Naibu Kamishna Carlos Haule, (Rukwa), Naibu Kamishna Julieth Sagamiko (Manyara), Naibu Kamishna Albert Rwelamila (Kilimanjaro) na Naibu Kamishna Paul Eranga (Mwanza)

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako