Nyingine

Kamati ya saa 72 kuhusu rufaa ya Simba kwa Kagera yaleta neema!!!

Mohamed Fakhi picha hii ni wakati akiwa mchezaji wa Simba

Simba walipeleka malalamiko hayo katika bodi ya Ligi na kuomba ipitie ripoti za waamuzi ili kujulikana ukweli.

Leo April 13 kamati ya saa 72 chini ya mwenyekiti wake Hamadi Yahaya ilikaa na kujiridhisha kuwa Kagera walikiuka taratibu hizo kwa mujibu wa Kanuni Simba wamepewa point zote tatu za mchezo dhidi yao.

Kamati imejiridhisha kuwa mchezaji Mohamed Fakhi alioneshwa kadi za njano katika mchezo dhidi ya Majimaji, Mbeya City na African Lyon, hivyo hakustahili kucheza katika mchezo dhidi ya Simba uliyochezwa April 2 2017 uwanja wa Kaitaba na Simba ikapoteza kwa magoli 2-1.

SOMA NA HII:  Idara ya Habari (MAELEZO) Yapokea Msaada wa Vifaa Kutoka Ubalozi wa China

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako