Nyingine

Kama kweli Makonda alifeli kidato cha nne, simlaumu kwa anachokifanya

Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye, amesema kama yasemayo kuhusu elimu ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni kweli, hamlaumu kwa maamuzi yake mbalimbali ambayo yamekuwa yakikosolewa vikali na wananchi.

Akiongea na waandishi wa habari Jumanne hii jijini Dar es Salaam, Sumaye alidai kuwa Makonda amepewa cheo kikubwa ambacho elimu yake haikimudu.

“Kama ni kweli [Makonda] amefeli darasa la saba kabisa, form four akafeli zote kabisa, kama ni kweli hivi ulitegemea afanyeje? Aendeshe mkoa sawa sawa?” alihoji Sumaye.

“Kama hizi failure ni kweli, huo uwezo wa kubeba hata wilaya uko wapi? Kwahiyo mimi simlamu Makonda. Yule bwana kwenye uongozi kuna kitu kinaitwa level of incompetency,” ameongeza.

Amedai kuwa huenda katika nyadhifa za chini Makonda alionekana kufanya vizuri hali iliyopelekea kupandishwa daraja haraka hadi kufikia kwenye kiwango ambacho hana uwezo nacho.

“Maana kama umefika mahali unavamia vituo vya habari, anakwenda waziri anayehusika na sekta hiyo anasikitika, anaeleza maelezo yale ambayo tumeyasikia sisi kwenye mitandao mengine mimi siwezi hata kuyarudia lazima kuna tatizo.”

Sumaye amesisitiza kuwa Makonda amefika mwisho wa uwezo wake.

Makonda amekuwa katika kipindi kigumu cha kukabiliwa na tuhuma nzito za kumiliki vyeti vinavyotajwa kuwa vimetokana na jina la mtu mwingine , aliyefaulu mtihani wa taifa wa kidato cha nne, Shule ya Sekondari ya Pamba, jijini Mwanza.

SOMA NA HII:  Kuwa mkweli! Jina gani umetumia ku-save namba ya simu ya mama yako?

Ijumaa ya wiki iliyopita, alijiongezea mzigo wa kashfa alipofuatana na polisi wenye silahausiku na kuvamia kituo cha habari cha Clouds Media, kilichopo Mikocheni, na kutaka kulazimisha kurushwa kipindi cha Shilawadu kwa namna atakavyo.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.