Sambaza:

Je! Ni kitu gani cha kwanza kufanya unaposikia email notification kwenye simu yako?

Wengi wetu, tunaangalia barua pepe zetu kwenye simu za mkononi kwanza. Sasa, ripoti inasema kwamba zaidi ya nusu ya barua pepe ulimwenguni pote zilizotumwa ndani ya mwaka 2017 zimesomwa kwenye simu za mkononi na nakubaliana na jambo hili.

SOMA NA HII:  Facebook kufanya utafiti ili kuboresha habari zake

Kwa takwimu, karibu 55% ya barua pepe ulimwenguni pote hufunguliwa katika mazingira ya simu ambayo ni mengi zaidi kuliko webmail (28%) na desktop (16%).

Matokeo ya ufunguaji wa barua pepe kwa njia ya simu yamebadilika kwa kasi kubwa ukilinganisha na mwaka 2012 ambapo ilikuwa 29%.

Binafsi, ninatumia simu ya mkononi kusoma na kupitia barua pepe zangu – lakini ikiwa nataka kujibu, ninafanya hivyo kwenye laptop yangu.

Je, ni sawa na wewe?

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako