Kadi ya NMB MasterCard inaruhusu manunuzi mtandaoni ?


Siku za karibuni nimekuwa nikikutana na maswali mengi kuhusu NMB MasterCard, baadhi ya maswali ni kama kadi ya NMB MasterCard inaruhusu manunuzi mtandaoni, wengine wanalalamika wamejalibu kununua bidhaa mtandaoni lakini hii kadi hairuhusu kukamilisha malipo ..na mara nyingi huwaletea ujumbe kuwa wamekosea kuandika namba za kadi (wakati wamezinakili vizuri)….Swali lililofanya nione umuhimu wa kuandika makala hii ni kutoka kwa mdau ambaye ameniuliza je ni kweli kadi hizi ni MasterCard ? na kama ni MasterCard afanye nini kukamilisha mchakato wa malipo mtandaoni?

NMB MasterCard

Jibu la maswali yote hayo ni rahisi, ni kweli NMB MasterCard inafaa/inaruhusu kufanya malipo mtandaoni kwenye masoko kama ebay, amazon na nk. Unachotakiwa kufanya ni kufungua akaunti ya Paypal ili uweze ku_link kadi yako, nenda kwenye tawi la NMB uwaeleze shida yako ili wairuhusu kadi iweze kufanya miamala mtandaoni – Kwa kujaza fomu maalum. Kwa kuwa watu wengi wanapata shida na matumizi ya NMB MasterCard nimeona ni vyema kuelezea kadi hii kwa undani zaidi.

NMB MasterCard ni nini ?

NMB MasterCard ni kadi mpya ya benki ya NMB inayomuwezesha mteja kupata huduma kama kutoa fedha kwenye ATM ya benki yoyote, kununua bidhaa au kulipia huduma wakati wowote na mahali popote duniani palipo na nembo ya MasterCard.

Tofauti gani iliyopo kati ya kadi ya zamani na ya MasterCard?

Kadi ya zamani mteja ana uwezo wa kuchukua fedha yake kwenye ATM za NMB pekee na hana uwezo wa kufanya manunuzi au kulipia huduma popote pale. Kwa kutumia NMB MasterCard, mteja anaweza kutumia ATM za NMB na zisizo za NMB zenye nembo ya MasterCard kuchukua fedha. Vilevile, ana uwezo wa kufanya manunuzi ya bidhaa madukani na kulipia huduma popote pale palipo na nembo ya MasterCard.

Nawezaje kupata NMB MasterCard?

Ili kupata NMB MasterCard, ni lazima uwe na akaunti na benki ya NMB. Tembelea tawi lolote la NMB na ujaze fomu ya maombi ili kupata kadi.

NMB MasterCard ina faida zipi?

NMB MasterCard ni rahisi kutumia. Mteja wa NMB ana uwezo wa kupata fedha zake mahali popote duniani inapokubalika MasterCard ikiwa ni pamoja na kwenye ATM na mashine za kulipia bidhaa madukani. Ni rahisi kubeba kuliko fedha. Ni kadi salama kutokana na teknolojia iliyotumika kuitengeneza.

Kuna vigezo gani vinavyotumika ili mteja aweze kuchagua kati ya kadi hizi?

Ili kupata kadi ya NMB World MasterCard, unatakiwa kutumia zaidi ya Tsh 4.5 milioni kwa mwezi kwa manunuzi ya kwenye mashine za ATM na nyinginezo zinazokubali malipo kwa mtandao wa MasterCard. NMB Titanium MasterCard, unatakiwa kuwa na matumizi yasiyopungua Tsh1.5 milioni kwa mwezi na kwa kadi ya NMB Tanzanite MasterCard hakuna kikomo cha kiwango cha matumizi.

Kuna faida nyingi za kuwa na MasterCard  ikiwa ni pamoja na usalama kwa manunuzi ndani na nje ya mtandao kupitia teknolojia ya MasterCard secure code, Chip na Pin, inakubalika kimataifa, uwezeshaji wa direct funds receipt kupitia huduma ya kutuma fedha ya MasterCard na upatikanaji wa punguzo na Ofa maalum kupitia program ya MasterCard PRICELESS

One Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *