Nokia na HMD Global wametoa vifaa vichache vya Android hadi sasa, lakini bado hatujaona simu yenye uwezo wa hali juu kutoka kwenye listi ya simu za kampuni hiyo. Sasa Subira hiyo inaonekana imefikia mwisho.

HMD inatuma mialiko ya tukio litakalo fanyika mnamo Agosti 16 huko London. Mwaliko hausema moja kwa moja kuwa Nokia 8 itakuwa simu ya mkononi itakayozinduliwa siku hiyo, lakini kuna uvumi unaonyesha kuwa simu mpya ya kisasa kutoka Nokia itazinduliwa karibuni, na mpaka sasa tukio litakalo fanyika London inaonekana kama sehemu sahihi na ya uhakika kuzindua simu hiyo.

SOMA NA HII:  Ifahamu simu ya Google Pixel 2 XL bei na Sifa zake

Kuna vipengele mbalimbali vinavyotarajiwa kuwepo kwenye simu ya Nokia 8.Inasemekana kuwa na kioo(display) ya 5.3-inch na resolution ya 2560  1440 na itakuwa na processor  ya Qualcomm Snapdragon 835, inatarajiwa kuwa na RAM ya hadi 6GB, na kamera mbili za nyuma zenye megapixel 13 na lenses za Carl Zeiss .

Kama uvumi huu utakuwa kweli, hii itakuwa moja ya simu za kisasa unazoweza kununua. Swali ni, Je! Nokia na HMD Global wataipa nguvu ya kutosha ili kupata mauzo mengi? Je, una mpango wa kununua Nokia 8?

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako