Jinsi ya Kuzuia Simu ya Android Kujua Eneo Ulilopo


Je, unajiuliza ni kiasi gani cha taarifa za eneo ulilopo Android imeripoti? Naam, angalia jinsi Google inavyojua kuhusu wapi ulipokuwa kwa kubofya kiungo hiki.

Ni jambo ambalo mwanzo lilikuwa linavutia zaidi lakini sasa linazua utata kidogo. Hiyo ni Google tu, na wako wazi juu ya jinsi wanavyotumia taarifa zako. Je, ni vipi kuhusu apps zingine zote ambazo umezipa ruhusa ya kuangalia eneo gani ulilopo ? Hapa tutazungumzia jinsi ya kuzuia uwezo wa apps kujua eneo ulilopo, na pia jinsi ya kuzuia kabisa simu yako kutuma maelezo ya eneo ulilopo, hata kwa Google.

Zuia Apps Binafsi Kujua Eneo Ulilopo

Unaweza kuona orodha ya apps ambazo kwa sasa zina uwezo wa kufatilia maelezo ya eneo ulilopo kwa kwenda kwenye Settings > Location kisha shuka chini. Kwa bahati mbaya, huwezi kuondoa ruhusa hizi kwa njia ya kawaida, labda kama app husika ina chaguo hilo ndani ya mipangilio yake.

Usiogope, ni kazi ndogo.

Pakua AppOps kutoka Google Play Store.

Ukimaliza ku-install, fungua app ya AppOps. Chagua app ambayo unataka kuizuia kufatilia eneo lako, na ubadilishe Location kuwa Off. Ni hayo tu!

Kuzuia Kabisa Ufatiliaji wa Eneo Ulilopo

Hii inaweza kuwa ngumu kidogo. Je upo tayari?

Nenda kwenye Settings > Location. Juu kabisa ya skrini, weka Location kuwa Off. Umemaliza ! Sawa… pengine tulimaanisha ni “rahisi”, sio ngumu…

Hitimisho

Kuruhusu apps kujua eneo ulilopo inaweza kuboresha utendaji wa baadhi ya apps. Google Maps, kwa mfano, ni muhimu sana ikiwa unairuhusu kujua wapi ulipo. Hata hivyo, ni muhimu kudhibiti kiwango cha taarifa za kibinafsi ambazo unasambaza kwenye apps mbalimbali, hasa ikiwa huelewi kwanini app husika inataka kujua wapi ulipo.

Je, una maoni gani kuhusu kushirikisha eneo ulilopo kwa apps na makampuni? Je! Unazuia kiasi gani maelezo ya eneo ulilopo?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA